BONANZA LA MAADHIMISHO YA MIAKA 63 YA UHURU WA TANZANIA BARA MANISPAA YA MOROGORO LAFAANA
KUELEKEA Maadhimisho ya Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara, watumishi wa Manispaa ya Morogoro na Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro wameshiriki michezo mbalimbali ikiwa ni kuelekea sherehe za miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Michezo hiyo imefanyika Disemba 8,2024 katika Kiwanja cha Mpira shule ya Msingi Mwere iliyopo Kata ya Kingo ikijumuisha michezo ya mpira wa Miguu , Netball na kuvuta kamba, karata ,bao n.k.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa michezo hiyo, Afisa Tawala Wilaya ya Morogoro akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Ndg. Hilary Sagara, amesema kuwa michezo ni afya hivyo kuelekea miaka 63 ya Uhuru muhimu kuimarisha afya ili kuendelea kuleta maendeleo.
“Michezo ni afya hivyo kuelekea katika maadhimisho ya miaka 63 ya uhuru wa wa Tanzania Bara tumeona ni vyema tukawa na michezo ,kwanza inakutanisha jamii, kubadilishana ubunifu wa kiutendaji lakini michezo inaimarisha afya zetu tutakwenda kuwatangaza washindi waliofanya vizuri katika michezo hii siku ya kilele cha maedhimisho Desemba 09-2024" Amesema Sagara.
Katika hatua nyengine, Sagara,amesema mwakani watahakikisha kunakuwa na michezo mingi zaidi ya hii ambayo imefanyika kwani zipo changamoto walizoziona na watazifanyia kazi katika maadhimisho ya miaka 64 ya Uhuru ya mwakani 2025.
Mdahalo wa miaka 63 ya uhuru utakaofanyika Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Disemba 9,2024.
Post a Comment