DIWANI NDWATA AWAPONGEZA VIONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA USHINDI WA KISHINDO NA KUWAAHIDI KUWAKATIA BIMA ZA AFYA
DIWANI wa Kata ya Kihonda Maghorofani, Mhe. Hamis Ndwata , amewapongeza viongozi wapya wa Serikali za Mitaa na kuwaasa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi, ikiwa ni pamoja na kusimamia mapato, miradi ya maendeleo, na kuwa sauti ya wananchi kwa kusikiliza kero zao.
Ndwata,ameyasema hayo katika Sherehe za kuwapongeza viongozi hao iliyofanyika Desemba 13-2024 katika Ukumbi wa Shule ya Wesley iliyopo Kihonda Maghorofani.
Aidha, Eng. Ndwata, amewapongeza viongozi hao na kuwaasa kuzingatia majukumu yao muhimu katika utawala wa Serikali za Mitaa.
Hata hivyo,amesisitizia kwamba viongozi hawa wanapaswa kuhakikisha mikutano ya kijamii inafanyika, kutekeleza miradi ya maendeleo, kusimamia mapato na matumizi, pamoja na kutatua migogoro mbalimbali, ikiwemo migogoro ya ardhi.
Mbali na pongezi hizo,ameweza kugawa vyeti vya shukrani kwa Viongozi wote ikiwemo Wenyeviti, Mabalozi, Viongozi wa Chama ,pamoja na wale wote waliofanikisha ushindi wa kishindo katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Mbali na vyeti vya pongezi, pia Eng. Ndwata,ameahidi kugawa bima za afya kwa Wenyeviti wote wa Serikali za Mitaa, Mabalozi wote pamoja, Viongo wa Chama pamoja na Wazee wa Kata hiyo .
Aidha,amesema kuwa nia kutoa bima hizo ni kuweza kuwasaidia viongozi hao kupata huduma ya afya uhakika na kirahisi katika Vituo mbalimbali vya afya vilivyopo hapa nchini .
Kwa upande wa Viongozi wa Serikali za Mitaa, ambaye jina lake limehifadhiwa, kwa niaba ya viongozi wenzake, wameshukuru jitihada za Diwani Eng. Ndwata kwa ahadi yake ya kuwakatia Bima ya Afya huku wakiwasii viongozi wengine kuiga mfano huo.
Post a Comment