Header Ads

AFISA UCHAGUZI MANISPAA YA MOROGORO AKUTANA NA WADAU WA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA PAMOJA NA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA





Viongozi wa Vyama vya Siasa pamoja na Wadau wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Manispaa ya Morogoro wamekutana  kujadili mambo mbalimbali ikiwa ni Pamoja na kukumbushwa  kuweka mawakala wao katika vituo vya kujiandikishia na ujazaji kamili wa wadhamini  kuelekea  uandikishaji wa  Wapiga kura  utakaofanyika tarehe 11-20 mwezi Oktoba 2024.

Akizungumza kwenye kikao hiko  Oktoba 08-2024 , Msimamizi msaidizi wa Uchaguzi kwa niaba ya Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi Manispaa ya Morogoro, Christopher Komba,  amesema lengo la kikao hiko ni kuwakumbusha vyama vya siasa kuwa wanao wajibu na haki ya kuweka mawakala wao katika vituo vya kujiandikishia  wapiga kura Pamoja na kuwahamasisha wanachama wao kujiandikisha katika daftari la  wapiga kura.


“Tarehe 11-20 Oktoba 2024  tunakwenda kuanza uandikishaji wa  wapiga kura,ni vema sasa tumeona tuwashirikishe wadau na viongozi wa vyama vya siasa vyote ili kuhamasisha wanachama na wafuasi wenu waweze kujiandikisha , tumeitana ili kukumbushana mambo muhimu ili uchaguzi wetu uwe huru naa wa haki " Amesema Komba .


Naye Afisa Uchaguzi Manispaa  ya Morogoro, Shabani Duru,amesema vituo vya kujiandikisha vitafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni 

Duru amesema zoezi la kujiandikisha llitaanza tarehe 11-20 mwezi Oktoba hivyo wananchi wajitokeze kwa wingi kujiandikisha.



No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.