Header Ads

KAMATI YA FEDHA NA UONGOZI MANISPAA YA MOROGORO YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO







KAMATI  ya Fedha na Uongozi  Manispaa ya Morogoro  ikiongozwa na Meya wa Manispaa  Mhe. Pascal Kihanga pamoja na timu ya wataalaam wa Manispaa ya Morogoro  imefanya Ziara ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo Agosti 21-2024 kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024-2025.

Hata hivyo Wajumbe wameridhishwa na utekelezaji wa Miradi hiyo ambapo wamepata taarifa za Miradi hiyo zilizofafanua muda , mapokezi ya Fedha,kiasi cha Fedha kilichopokelewa,kilichotumika na kilichobaki Kwa baadhi ya Miradi  sambamba na hali ya utekelezaji wa kila Mradi.

Akizungumza kwa niaba ya Kamati ya Fedha na Uongozi, Mhe.Pascal Kihanga ambaye ndiye mwenyekiti wa Kamati hiyo, ametoa pongezi kwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha nyingi za miradi ya maendeleo hususani Manispaa ya Morogoro ikiwa na lengo la kurahisisha upatikanaji wa huduma za jamii kwa wananchi.

Aidha, Mhe .Kihanga,ameipongeza timu nzima ya Menejimenti ya Manispaa inayoongozwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Emmanuel Mkongo kwa kufanya kazi kwa ustadi mkubwa huku akiwataka waendelee na kasi kubwa ya kufanikisha miradi ya maendeleo inakamilika kwa wakati.

Katika Ziara hiyo Wajumbe wametembelea  Miradi mbalimbali ya Maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara ya tactic ili kujionea maendeleo ya mradi huo, shule kongwe ambazo zinahitaji kufanyiwa maboresho, Soko la machinga Complex Fire, nyumba ya kurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Choo cha Stendi ya SGR , pamoja na shule mpya ya Sekondari ya Sultan Area inayojengwa eneo la Kiegea A Kata ya Kihonda.





No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.