MWENYEKITI UMOJA WA WAZAZI CCM TAIFA AIPA KONGOLE MANISPAA YA MOROGORO
MWENYEKITI wa Umoja wa Wazazi CCM Taiafa na Mjumbe wa Kamati Kuu Taifa Ndug.Fadhili .Maganya ameipongeza Manispaa ya Morogoro kwa kutumia fedha za mapato ya ndani kukamilisha Kituo kikubwa cha kisasa cha Afya Kata ya Tungi.
Pongezi hizo amezitoa katika ziara yake ya kikazi ya siku 5 Mkoani Morogoro akitembelea Kituo hicho cha afya Tungi pamoja na Shule ya Msingi Jitegemee Oktoba 02-2024 na kujionea Manispaa ilivyojipanga kuwahudumia wananchi wake kwenye suala zima la afya na elimu.
Aidha,amelipongeza baraza la Madiwani Manispaa ya Morogoro linaloongozwa na Meya wa Manispaa Mhe.Pascal Kihanga, pamoja na Timu ya Wataalamu inayoongozwa na Mkurugenzi Emmanuel Mkongo kwa kutekeleza miradi hiyo kwa ubora na viwango vya juu.
"Nimezunguka kote katika ziara yangu ya kikazi,nimeo majengo makubwa ya kisasa ya Vituo vya Afya lakini yote yametumia fedha za Serikali Kuu kwa hapa kwenu nimeona toafuti kwa kutumia fedha za mapato ya ndani hongereni sana na mmeupiga mwingi sana" Amesema Maganya.
Hata hivyo, Mwenyeketi wa Jumuiya na Mjumbe wa Kamati kuu ,Ndug. Maganya, ametoa rai kwa jamii kama wazazi kuitunza na kuilinda miradi yote inayotekelezwa kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro,Mhe.Pascal Kihanga, amemshukuru Mwenyekiti huyo wa Wazazi CCM Taifa na viongozi aliyoambatana nao kwa kutembelea Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro na kuona mradi wa Kituo cha Afya Tungi pamoja na miradi ya elimu ikiwemo Shule ya Msingi Jitegee iliyopo Kata ya Chamwino.
Akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa Kituo cha Afya kwa mgeni rasmi,Mtendaji wa Kata ya Tungi,Laurent Masanja, kwa niaba ya Mkurugenzi ameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Rasi Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuthamini wananchi wa Halmashauri hiyo hususani wakazi wa Kata ya Tungi.
Post a Comment