MSIMAMIZI WA UCHAGUZI MANISPAA YA MOROGORO AWATAKA WAANDIKISHAJI KUZINGATIA KANUNI NA MIONGOZO
MSIMAMIZI wa Uchaguzi Manispaa ya Morogoro,Emmanuel Mkongo, ametoa rai kwa waandikishaji orodha ya wapiga kura kuzingatia mafunzo watakayofundishwa ikiwemo kuzingatia kanuni za Uchaguzi wakati wa zoezi la uandikishaji linalotarajiwa kuanza tarehe 10 hadi 20 mwezi Oktoba 2024.
Kauli hiyo ameitoa Oktoba 07-2024 katika Ukumbi wa Tanzanite Hall.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya waanikishaji wa orodha ya wapiga kura,Mkongo, amewapongeza waandikishaji hao kwa kuteuliwa kufanya kazi hiyo na kuwaahidi kuwapa ushirikiano pale watakapohitaji, pia amewataka kufanya kazi kwa juhudi ili kufikia malengo na kufanya wananchi wengi kushiriki kupiga kura siku ya tarehe 27 Novemba 2024.
Aidha,Mkongo, amewasihi waandikishaji hao kufuata taratibu na kuuliza pale wanapokosa majibu na sio kufanya kwa utashi wao.
Waandikkshaji hao wameapa na wako tayari kwa kuanza zoezi la uandikishaji,kwa kuzingatia mafunzo waliyopewa kwa kufuata kanuni na miongozo ya uandikishaji.
Aidha, waandikishaji hao wa uchaguzi wamekula viapo vya utii, uadilifu, uaminifu na kutunza siri wakati na baada ya zoezi hilo la uchaguzi.
Post a Comment