Header Ads

OPCHUO KIKUU HURIA (OPEN UNIVERSITY) KIMEENDELEA KUPIGA HATUA KWA KUIMARISHA MIFUMO YA UFUNDISHAJI-DC KILAKALA



CHUO kikuu Huria (Open University) kimeendelea kupiga hatua kwa kuimarisha zaidi mifumo yake ya utendaji na kufundisha huku msisitizo mkubwa ukiwa katika matumizi ya TEHAMA.

Hayo yalisemwa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro ,Mhe.Mussa Kilakala, Oktoba  14-2024 akiwa mgeni rasmi wakati wa  maadhimisho ya miaka 30 ya chuo hicho tangu kuanzishwa kwake Desemba 1992 kweye Viwanja vya Stendi ya zamani ya Daladala Mjini Kati Manispaa ya Morogoro  ambapo kilele  cha maadhimisho hayo kinatarajiwa kuwa mwezi Novemba 05-2024  kwenye uwanja wa Lake Tanganyika Mkoani Kigoma.

DC Kilakala, amesema  mifumo ya elimu imekuwa ikiimarishwa mara kwa mara ili kuendana na mabadiliko ya ulimwengu katika nyanja za kiuchumi, kisiasa, teknolojia na kijamii.

"Mabadiliko haya yanailazimu serikali kufanya mapitio ya sera ya elimu kuanzia ngazi ya msingi ili kuiwezesha nchi kupiga hatua. Tunajua kuwa hili pia ni kipaumbele kwa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na chuo hiki kina jukumu la kubeba dhamana ya haya mabadiliko yanayofanyika kwa kuwa ni wadau muhimu wa mabadiliko hayo. Lengo ni kuwa na aina ya elimu itayozalisha wahitimu wenye ujuzi, maarifa na uwezo wa kujitegemea katika kujiajiri na kuajiri wengine,”Amesema DC Kilakala.

Pia,DC Kilakala,amesema maadhimisho hayo yameenda sambamba na kumbukizi ya miaka 25 ya Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere huku akiwataka watanzania kuendelea kudumisha amani ,upendo na mashikamano na kufanya kazi kwa bidii ili kuzidi kulijenga Taifa la Tanzania linaloongozwa na Rais wa Awamu ya Sita ,Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Aidha,DC Kilakala,amechukua fursa hiyo ya hadhara kuwaomba wananchi waendelee kujitokeza kwa wingi katika zoezi linaloendelea la uandikishaji wa orodha ya wapiga kura ili kuchagua viongozi wanaowataka watakaoweza kuleta maendeleo katika maeneo yao.

Naye Mkurugenzi wa Kito cha Elimu ya juu Chuo Kikuu Huria cha Open University Mkoa wa Morogoro,Dkt. Christopher Getera, , amesema kitendo cha serikali kuendelea kuchangia maendeleo ya chuo ni kuthamini machango wake kwa jamii na hivyo kukifanya chuo  kiendelee kutimiza wajibu wake wa kutoa elimu kwa wanachuo huku wakiwa wanaendelea na shughuli zao huko huko walipo.

Dr.Getera,amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Morogoro kuwa mgeni rasmi wa maadhimisho ya miaka 30 ya utoaji wa elimu ya chuo hicho huku akimuahidi kumpa ushirikiano ili kuendelea kuunganisha nguvu ya Serikali pamoja na wadau wa elimu ikiwemo Chuo hicho.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.