JUMUIYA YA WAZAZI CCM MKOA WA MOROGORO YAPATA SAFU YA VIONGOZI WAKE .
JUMUIYA ya Wazazi CCM mkoa wa Morogoro hatiamaye imepata safu ya viongozi baada ya mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Dkt. Rose Rwakatare kuitisha baraza rasmi na kuteua wajumbe wa baraza hilo na wajumbe wa kamati ya utekelezaji kwa ridhaa wajumbe wa baraza la mkoa.
Wajumbe hao wamechaguliwa Aprili 16/2023 katika Kikao cha kwanza cha Baraza la Kawaida la kazi na kupeana maelekezo ya utendaji kazi na dira ya Jumuya ya Wazazi katika Ukumbi wa Mikutano wa CCM Mkoa.
“Kwasasa safu ya Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Morogoro imekamilika ambapo ina wajumbe wa kamati ya utekelezaji wajumbe wa kamati tendaji lakini pia wajumbe wa baraza rasmi, sasa naomba nitoe dira kuwa mkoa wa Morogoro Jumuiya ya Wazazi inakwenda kusimamia mambo yake makuu matano ambayo ni elimu, malezi, afya, mazingira na uchumi katika Mkoa wetu wa Morogoro " Amesema Rwakatare.
Aidha, amesema Jumuiya ya Wazazi CCM inadili na mambo hayo matano na kama ilivyo kwa sasa hali ya mmomonyoko wa maadili umekithiri sana hivyo inakwenda kudili na na suala hilo na hayo mengineyo.
Upande wa Katibu wa Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Zuberi Mtelela, amesema kwa kushirikia na makatibu wote wa Kata zote katika Mkoa wa Morogoro watahakikisha wanatoa mafunzo ya uongozi kupitia kamati za utekelezaji na kamati za wilaya.
Mtelela, amesema Jumuiya ya Wazazi inakwenda kuandaa mpango kazi wa miaka mitano kuhakikisha majukumu yake hayo inayafanya kifasaha na kurejesha heshima na hadhi ya jumuiya na kufanyakazi iliyotukuka kuhakikisha chama Cha Mapinduzi kinapata ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu wa 24/25″.
Wajumbe wa Baraza walioteuliwa katika kikao hicho cha kwanza cha baraza la kawaida la kazi ni Farida Zaharani, Mathias Msimbe na Juma Libawa .
Katika upande wa Wajumbe Kamati ya Utekelezaji ni Teddy Lugendo, Anna Mtenga, Hao Kipolelo na Juma Libawa.
Post a Comment