BARAZA LA MADIWANI ROBO YA TATU MANISPAA YA MOROGORO LAFANYIKA APRILI 27/2023.
BARAZA la Madiwani Manispaa ya Morogoro ya robo ya tatu kipindi cha Januari hadi Machi 2023 limefanyika leo Aprili 27/2023 katika ukumbi wa Mikutano Ofisi Kuu ya Manispaa.
Akifungua mkutano huo uliohudhuriwa pia na Viongozi wa vyama vya siasa, Wakuu wa Idara na Vitengo, Mwenyekiti wa Baraza ambaye pia ni Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mhe. Pascal Kihanga, amesema ni mkutano wa kawaida kwa lengo la kuthibitisha taarifa za kawaida za utekelezaji wa Kamati za Kudumu za Halmashauri.
Amesema taarifa hizo ni za utekelezaji kwa kipindi cha robo ya tatu na zitawasilishwa na Wenyeviti wa Kamati hizo za Kudumu kwa lengo la kuzijadili ili changamoto ziweze kutatuliwa kwa wakati na ufanisi.
Pamoja na kuwasilishwa kwa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, Meya Kihanga , ameitaka Halmashauri hiyo kuhakikisha inasimamia vema miradi ya maendeleo katika sekta ya elimu, afya, barabara, maji na miundombinu mingine ili kuleta tija kwa Halmashauri na wananchi kwa ujumla.
Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro , Ally Machela, ameahidi kutekeleza maelekezo yaliyotolewa na Wajumbe wa Baraza ili kuleta tija kwa Halmashauri.
Machela, amesema viporo vya miradi yote ambayo haikukamilika katika mwaka wa fedha 2022/2023 kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha huo vitakamilika vyote hususani viporo vya maboma ya madarasa pamoja na kuboresha huduma za afya ikiwamo kusambaza vifaa tiba Vituo vya afya na Zahanati.
Taarifa zilizowasilishwa ni utekelezaji wa Kamati ya Maadili ya Madiwani, Kamati ya Huduma za Uchumi Afya na Elimu, Kamati ya Mipangomiji na Mazingira, Kamati ya Kudhibiti UKIMWI pamoja na Kamati ya Fedha na Uongozi.
Post a Comment