BEGA KWA BEGA NA MAMA SAMIA YAADHIMISHA SHEREHE ZA MIAKA 59 YA MUUNGANO, MGANGA MKUU MANISPAA YA MOROGORO ATOA NENO
TAASISI ya Bega kwa Bega na Mama Mkoa wa Morogoro ,imeadhimisha sherehe za miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kushiriki katika michezo mbalimbali pamoja na kuzungumzia miradi ya maendeleo inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Maadhimisho hayo yamefanyika katika Viwanja vya michezo Shule za Msingi Msamvu A na Msamvu B Aprili 26/2023 ambapo Mgeni rasmi alikuwa Mganga Mkuu wa Manispaa ya Morogoro Dr. Charles Mkumbachepa.
Akizungumza na wananchi waliojitokeza katika maadhimisho hayo, Dr..Mkumbachepa, amewataka Wananchi wa Mkoa wa Morogoro kuzidi kudumisha amani na kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo.
Dk.Mkumbachepa,amesema kuwa kila Mtanzania ana mchango wake katika kufikisha maendeleo ya miaka 59 ya Muungano huku amani ikiwa chachu ya mafanikio kwa miaka hiyo ya Muungano.
Aidha, amesema kuwa thathmini inaonesha jinsi gani Tanzania ilivopiga hatua, hivyo kuna kila sababu ya kujua ni mambo yapi yamefanywa na Serikali chini ya Uongozi wa Awani ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Hata hivyo, amewataka wazazi na walezi kulipa kipaumbele suala la malezi kwa watoto.
“Naomba sana suala la malezi mliangalie vizuri watoto walelewe kimaadili na viongozi kusimamia utunzaji wa mazingira” Amesema Dr. Mkumbachepa.
Mwisho, ameipongeza Taasisi ya Bega kwa Bega na Mama huku akiahidi Serikali kuendelea kuwapa ushirikiano pale wanapo hitaji kujua miradi inayotekelezwa kwa ajili ya kuisemea.
Naye Mratibu wa Maadhimisho hayo kutoka Taasisi ya BEGA KWA BEGA NA MAMA, Ruth Mateleka, amesema kwa kipindi cha miaka 61 tangu taifa lipate uhuru limepiga hatua kubwa na sasa hata wakati wa miaka 59 ya Muungano Maendeleo ni makubwa sana
“Tanzania imepiga hatua kwa kiasi kikubwa sana kipindi kile tulikuwa tunasafiri siku nzima kwa sababu ya barabara, lakini sasa hivi ni rahisi sana, lakini miradi mikubwa inataekelezwa kama mradi wa Umeme wa Mto rufiji, ujenzi Hospitali za Rufaa na Wilaya pamoja na Vituo vya afya, Ujenzi wa Madarasa , Wodi za wakina mama na watoto , ujenzi wa mradi wa treni ya Umeme SGR yote haya Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan ameyafanya kwa kwa kipindi kifupi akiwa madarakani ” Amesema Mateleka.
Katika maadhimisho hayo zawadi kemkem zilitolewa kwa wana michezo waliofanya vizuri pamoja na vyeti vya shukrani kwa Viongozi.
Katika Maadhimisho hayo, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alielekeza maadhimisho sherehe za miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yafanyike katika ngazi ya mikoa kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi.
Ikumbukwe kuwa Muungano wa Taganyika na Zanzibari uliasisiwa tarehe 26 Aprili, 1964 takribani miaka 59 iliyopita, na Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere, na Hayati Abeid Aman Karume.
Post a Comment