Header Ads

EGG -TANZANIA YAFUTURISHA ZAIDI YA WATU 400 KATIKA MFUNGO WA RAMADHANI


TAASISI ya kiraia ya EGG -Tanzania, yenye makao yake Manispaa ya Morogoro imefuturisha zaidi ya watu 400  ikiwa ni ishara ya shukurani na pia kudumisha umoja na mshikamano. wafanyakazi hao.


Akizungumza wakati wa hafla huyo, Mkurugenzi wa EGG- Tanzania, Jumanne Mpinga, amesema hafla hiyo imekuwa ya baraka mno ukizingatia kuwa kipindi hiki waislamu kote nchini wanaendelea na mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani hali kadhakika waumini wa dini ya kikristo wao wakiwa wamemaliza  mfungo wao wa Kwaresma na kusherekea Sikukuu ya Pasaka.

"Sisi kama EGG -Tanzania tunaamini mshikamano mahali pa kazi ndio siri kubwa ya mafanikio yetu, hivyo hafla kama hizi ni muhimu sana katika kuendelea kuwaweka wananchi wetu na jamii tunazo zisaidia  pamoja na kudumisha moyo wa upendo, umoja na mshikamano miongoni mwao, sisi sio Taasisi ya Kidini bali tunafanya kazi na Jamii zote na makundi yote ikiwemo kusaidia huduma za elimu, maji kwa kuchimba visima , kugawa Baiskeli kwa wanafunzi wanaoishi mbali na huduma za shule , haya yote tumekuwa tukiyafanya kwa lengo la kusaidia Serikali katika majukumu ya kuwatumikia Wananchi wake" Amesema Mpinga.

"Ujio wa viongozi wa Serikali na Chama katika hafla hii limetupa faraja kama Taaisis, namshukuru Diwani wa Kata ya Mindu Mhe. Zuberi Mkalaboko akimwakilisha Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mwenyekiti wa Wazazi CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Ndg. Salum Kipira na wajumbe wake pamoja na mashekhe kwa kukubali mwaliko wetu" Ameongeza Mpinga.

Aidha, Mpinga, amewashukuru Viongozi wa Serikali  na Viongozi wa vyama vya siasa kwa kuwa begakwa bega  lakini hususani katika jitihada zao za  bila kuchoka katika kuwatumikia wananchi huku akiweka matumaini kuwa  jitihada hizo na uchapakazi wao utaendelea kuiweka Tanzania katika ramani nzuri hususani katika suala zima la Utawala bora .

Naye Diwani wa Kata ya Mindu, Mhe. Zuberi Mkalaboko, ameishukuru Taasisi ya EGG -Tanzania kwa futari lakini kwa kazi kubwa wanazozifanya katika kusaidia jamii ,hivyo amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau kuhakikisha wananchi wanapata hudma bora.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Wazazi CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Ndg. Salum Kipira, amesema kwa kuwa Jumuiya yake inajihusisha moja kwa moja na masuala ya elimu, watashirikiana kuhakikisha kuwa maadili yakuwa makubwa na elimu inanyanyuka pamoja kutoa ushirikiana kama Viongozi wa kisiasa pala wanapohitajika.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.