MENEJIMENTI YA MANISPAA YA MOROGORO YARIDHISHWA NA KASI YA MABANDA YA MACHINGA FIRE.
MENEJIMENTI ya Manispaa ya Morogoro ikiongozwa na Mkurugenzi wa Manispaa, Ally Machela, imeridhishwa na kasi ya ujenzi wa Mabanda ya wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) katika eneo la Fire.
Akizungumza na Wakuu wa Idara na Vitengo, Machela, amesema ujenzi wa mabanda hayo unaenda kwa kasi kubwa hivyo , ametaka kamati ya ujenzi kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa wakati ili wafanyabiashara wafanye biashara kwa uhuru na katika eneo rafiki.
Machela ,amesema kuwa , Manispaa ya Morogoro kuna wafanyabiashara ndogondogo wengi hivyo kwa kutumia mapato ya ndani, Manispaa ya Morogoro itaendelea kuwalinda Machinga na kuwatafutia maeneo mbalimbali yaliyo rafiki ya kufanyia kazi.
"Manispaa yetu ya Morogoro kwa kushirikiana na Mkuu wetu wa Wilaya, Wabunge, Viongozi wa Siasa, wadau mbalimbali wa maendeleo, Wataalamu wa Manispaa, watendaji na wananchi tutaendelea kusimamia vyema wafanyabiashara wadogowadogo kuhakikisha wanafikia malengo kwani wao wana haki kama ilivyo watu wengine, hivyo Serikali imewatambua Kama kundi muhimu, kwahiyo wajibu wetu Viongozi kuwasimamia na kutatua changamoto zao" Amesema Machela.
Mwisho, amewataka Machinga kuendelea kuwasikiliza Viongozi wao kwani Serikali ipo bega kwa bega na wao kwa kutambua kundi hilo lina mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa Taifa.
Manispaa imetekeleza ujenzi wa Mabanda hayo ambayo Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe. Albert Msando, amekuwa mstari wa mbele kuhakiksha kero za Wamamchinga zinataturiwa.
Ikumbukwe kuwa Ujenzi wa mabanda hayo 4, yatakayo tumia jumla ya shilingi Milioni 200 hadi kukamilika kwake na kuwa moja ya vyanzo vya mapato vya manispaa.
Post a Comment