MANISPAA YA MOROGORO KUKAMILISHA UJENZI WA ZAHANATI 5 MWAKA WA FEDHA 2021/2022.
MANISPAA ya Morogoro ipo katika mpango wa kukamilisha ujenzi wa Zahanati 5 katika mwaka huu wa fedha wa 2021/2022.
Kauli hiyo imetolewa leo Februari 03/2022 na Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Ally Machela, katika Mkutano wa kawaida wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Manispaa wa Kilakala Soko Kuu la Chifu Kingalu.
Akizungumza katika Mkutano hu, Machela, amesema kuwa Manispaa imejiwekea utaratibu wa kufanya vikao viwili kila wiki ambapo menejimenti hujadili taarifa za mapato katika vyanzo vyote zikiwemo hospitali vituo vya afya na Zahanati jambo ambalo Wakuu wa Idara hushiriki na kutoa mawazo juu ya jitihada za ukusanyaji mapato.
Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Ally Machela,
“Kwenye makusanyo huwa tunakusanya kwa asilimia kubwa, hii imepelekea Manispaa kuweza kupeleka fedha katika miradi ya afya na ndio maana kwa sasa tupo katika kukamilisha Zahanti 5 katika mwaka huu wa fedha wa 2021/2022.
Aidha, amesema kuwa Manispaa kupitia mapato ya ndani wataendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kadri tunavyozidi kupata makusanyo na kutenga fedha zitakazo sukuma miradi kwa ajili ya kuwahudumia Wananchi.
Miongoni mwa Zahanati hizo ni pamoja na Zahanati ya Mbuyuni, Sultan Area, Kihonda Maghorofani, Kiwanja cha ndege, na Zahanati ya Tungi.
Post a Comment