DC MSANDO AZINDUA KAMPENI YA UPANDAJI WA MITI PEMBEZONI MWA VYANZO VYA MAJI BWAWA LA MINDU.
MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Albert Msando, amezindua rasmi kampeni ya upandaji miti pembezoni mwa vyanzo vya maji.
Zoezi hilo la uzinduzi limefanyika leo Februari 05/2022, Kata ya Luhungo, pembezoni mwa Bwawa la Mindu.
Akizungumza na wananchi waliojitokeza katika kampeni hiyo, DC Msando, amesema lengo la kupanda miti hio ni kulinda vyanzo vya maji.
Katika zoezi hilo lilojumuisha wadau mbalimbali wa Mazingira, DC Msando, akiambatana na Viongozi wa CCM Wilaya, Kamati ya ulinzi na usalama, wadau wa mazingira ikiwamo Bonde, MORUWASA, amewapongeza wananchi waliojumuka katika zoezi hilo la kampeni ya upandaji wa miti, huku akiongeza kuwa kampeni ya upandaji miti kwa kushirikiana na wanafunzi ni jambo la msingi kwani hivi ndio vizazi vijavyo na vinahitaji mazingira safi na salama.
“Watu wengi hawaelewi wanafikiri mazingira ni taka ngumu, maji taka au chupa za plastiki tu, mazingira ni kila kitu kinacho tuzunguka,hivyo tujitahidi kupanda miti ili kuiweka nchi yetu katika usalama. Wanafunzi na watu wengi hawaelewi kuwa juhudi kubwa zinazofanywa na serikali za kulinda mazingira" Amesema DC Msando.
DC Msando, ameendelea kusisitiza kuwa jitihada kubwa za Serikali ambazo zinafanywa kulinda mazingira ziungwe mkono na wananchi kwa ni jukumu la kila mmoja na sio kuitegemea NEMC peke yake.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro, Jeremia Dauson, amesema kuwa kama mnavyofahamu katika kipindi hiki tabia inabadilika, hivyo wazo la upandaji miti katika Manispaa yetu ya Morogoro ni zuri sana kwani itasaidia kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi na vyanzo vya maji kuwa salama.
Naye Kwa upande wa Mhandisi wa rasilimali za Maji, Bonde la Maji la Wami Ruvu, ,akimwakilisha Mkurugenzi wa Bonde la Wami, John Kasambili,amempongeza DC Msando kwa kazi nzuri anayofanya ya kuifanya morogoro kuwa ya ukijani.
“ Tunafanya hivi tukiamini kuwa mazingira bora yanamchango mkubwa sana katika ustawi wa jamii yetu na maendeleo yetu kwa ujumla" Amesema Kasambili.
Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Fikiri Juma, amewataka wananchi wa Manispaa ya Morogoro waache tabia ya kutupa taka hovyo wakiwa kwenye magari kwani kufanya hivyo ni makosa kisheria na inaharibu mazingira yetu kwa ujumla kwani mji unapokuwa msafi unafanya kuwa kivutio cha watalii na inaleta ustawina viumbe hai vyote.
Post a Comment