Header Ads

DC MSANDO , AKEMEA VIKALI MATUMIZI HOLELA YA VYOMBO VYA USAFIRI.


MKUU wa Wilaya ya  Morogoro, Mh Albert Msando amekemea vikali kuhusu matumizi mabaya ya vyombo vya usafiri ikiwemo na pikipiki, bajaji na daladala.

 Ameyasema hayo akiwa na waandishi wa habari, katika kikao cha uwasilishaji wa bajeti ya mwaka wa fedha wa 2022-2023 kilichofanyika katika Ukumbi wa Kilakala uliopo soko kuu [chifu kingalu] tarehe 10-2-2022.

 ambapo amealika wenye kiti wa vyombo vya usafiri ili wawe chachu ya kuzuia utumiaji huo wa kiholela wa vyombo vya moto, na amemuomba Mkurugenzi wa Manispaa kuzidi kutoa ushirikiano katika hili.

 ‘’Marufuku kuendesha kuendesha vyombo vya usafiri kinyume na sheria  na kwa upande wa bajaji tutahakikisha tunaweka stika ambapo stika nyekundu kwaajili ya bajaji za makodisho na stika nyeupe ni kwaajili ya bajaji za abiria’’ Amesema DC msando.

 Ameongeza kuwa hairuhusiwi kutolewa leseni za vyombo vya usafirishaji bila idhini ya Mkurugenzi, na mikakati ya kutenga eneo maalumu kwaajili  ya bodaboda inaendelea kufanyika ili kuzuia utokeaji wa ajali za mara kwa mara barabarani.

 ’Mkurugenzi ndo mwenye idhini ya kutoa leseni  na tunawapa onyo wale bodaboda walofunga barabara na kutishia kuharibu miundo mbinu ya serikali’’ Ameongeza DC  Msando.

 Pia, DC Msando, amempongeza meneja wa TARURA kwa kuunga mkono katika kusawazisha eneo la maegesho ya watu wa bajaji yalipo Soko Kuu Kingalu jirani na Mto Kikundi.

Mwisho ametoa siku saba kwa Vituo vyote vya mafuta, ( Petrol Station)  kukamilisha madai wanayodaiwa na Halmashauri ya kodi za huduma ( Service Levy) na amemtaka Mkurugenzi kufungia vituo ambavyo havitalipa fedha hizo.

     

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.