MANISPAA YA MOROGORO YAJA NA MPANGO WA KUKOMESHA UVAMIZI MAENEO YA WAZI.
MANISPAA ya Morogoro ipo mbioni kuweka alama za utambuzi wa maeneo yote ya wazi ikiwa na lengo la kukomesha uvamizi wa maeneo hayo.
Kauli hiyo imetolewa leo na Afisa Mipango Miji wa Manispaa ya Morogoro kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa, Emeline Kihunrwa, katika ziara ya wataalamu wa mipango Miji leo Februari 18/2022.
Akizungumza mara baada ya ziara hiyo kukamilika, Kihunrwa, amesema lengo la kuweka alama hizo za utambuzi ni kudhibiti uvamizi wa maeneo ya wazi ambayo Manispaa imeyatenga.
"Maeneo yetu ya wazi yanavamiwa , sasa tumeamua kuja na suluhisho la kuweka alama kubwa za utambuzi katika maeneo yote ya wazi, tunataka kuupanga mji wetu, bila kuwa na mpango wa matumizi na kuyatambua maeneno yetu ya wazi migogoro ya ardhi haiwezi kuisha na tukipanga na kuheshimu makubaliano yaliyowekwa katika maeneo haya ni wazi migogoro itapungua na ili kufanikisha hili tunaanza utekelezaji wa haraka " Amesema Kihunrwa.
Aidha, amesema kuwa wale wote ambao watavamia maeneo ya wazi yakiwa yamewekwa alama za utambuzi watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Aidha, alama ambazo wajumbe wamependekeza ni za kuweka majiwe ya Msingi wa Matofali yatakayokuwa na ujumbe wa makatazo ya wananchi kutumia maeneo hayo kuliko alama za ubaoa mabazo ni rahisi kuondokeka.
Miongoni mwa wajumbe waliohudhuria katika ziara na kufanya kikao cha kawaidia cha Wataalamu wa Mipango Miji ni pamoja na wataalamu wa ardhi kutoka Manispaa, TANESCO, ZIMA MOTO, TARURA, na wajumbe wengine.
Katika ziara hiyo ya wataalamu wa Mipango Miji , miongoni mwa maeneo yaliyotembelewa ni pamoja na Mtaa wa Kambi Tano Lukobe ambapo kuna maeneo ya wazi , eneo la Star City , Ofisi ya Kata ya Mafiga ambayo eneo hilo limejengwa majengo ya Umma ikiwemo Ofisi ya Kata na Kituo cha Polisi, eneo la kona ya Mafiga Sekondari ambapo kuna mmiliki wa nyumba aliyeomba kibali cha kubadili matumizi ya ardhi kuwa kituo cha mafuta, pamoa na eneo la Kichangani jirani na barabara ya kuingia Chuo Kikuu cha Jordan ambapo eneo hilo limeombewa kibali kubadili matumizi kujengwa Msikiti kutoka Taasisi ya Istiqama Islamic Foundation .
Post a Comment