MANISPAA YA MOROGORO KUKUSANYA BILIONI 10 MAPATO YA NDANI MWAKA WA FEDHA 2022/2023
HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro inatarajia kukusanya kiasi cha shilingi Bilioni 10 kupitia mapato ya ndani katika mwaka wa fedha wa 2022/2023.
Hayo
yamezungumzwa Februari 10, 2023, na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe.
Pascal Kihanga, wakati wa kuwasilisha rasmi Bajeti ya mwaka wa fedha wa
2022/2023 katika Mkutano maalum wa Bajeti wa Baraza la Madiwani la Manispaa ya
Morogoro katika Ukumbi wa Kilakala Soko Kuu la Chifu Kingalu Morogoro.
Akizungumza
na Waandishi wa habari, Kihanga, amesema Manispaa inakadiria kukusanya na
kutumia kiasi cha shilingi Tshs.84,974,512,600.00 ambapo kwenye mapato ya ndani
ni Tshs.10,754,563,600.00 , ruzuku ya mishahara na matumizi ya kawaida Tshs.84,891,140,000.00
na miradi ya Maendeleo ni Tshs.8,568,986,000.00.
Hata
hivyo, amesema Manispaa ya Morogoro , imeendelea na utoaji wa Mikopo ya
Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu kama kanuni inavyoagiza kuwa Halmashuri
kupitia mapato yake ya ndani kutenga asilimia 10.
Amesema
katika bajeti ya 2022/2023Manispaa ya Morogoro, ilitenga kiasi zaidi ya milioni
912,345,060.00 kwa ajili ya mkopo ya
uwezeshaji wa kiuchumi kwa Vijana, Wanawake na watu wenye ulemavu.
Katika ujenzi wa madarasa ,
Mhe. Kihanga, amesema Manispaa imetenga kiasi cha shilingi milioni 625 kwa
ajili ya umaliziaji wa maboma 50 ya madarasa ya shule za Msingi.
Katika huduma za afya, Manispaa
ya Morogoro imetenga kiasi cha Tshs.300,000,000.00 kwa ajili ya ukamilishaji Kituo
kimoja cha afya huku ikitenga shilingi milioni 200,000,000.00 kumalizia
miundombinu ya Zahanati 4 za Mji Mkuu, Kauzeni, Mafiga na Kihonda.
Mwisho, amewashukuru Viongozi
wa vyama vya Siasa, Viongozi wa Taasisi mbalimbali, Waheshimiwa Madiwani , wadau wa maendeleo, Wananchi pamoja
na Waandishi wa habari kwa kuhudhuria Mkutano huo muhimu ambapo amesema pamoja
na mambo mengine , bajeti hiyo imezingatia Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020 -2025 na mkakati wa kukuza Uchumi na kupunguza
Umasikini (MKUKUTA).
Naye
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Ally Machela, amewashukuru Wananchi wote waliohudhuria kikao
maalumu cha kupitisha mapendekezo ya mipango ya bajeti 2022/2023.
"Nawashukuru
sana Waheshimiwa Madiwani kwa maelekezo yenu ya msingi mliyoyatoa wakati wa
kujadili bajaeti hii kupitia kamati zetu za kudumu za Halmashauri, niwapongeze
Wananchi wote kupitia Mabaraza ya Maendeleo ya Kata na katika vikao
vilivyofanyika katika nyakati na ngazi mbalimbali ,kwa kujitokeza kwa wingi ,
waandishi wa habari, napenda kuwahakikishia mawazo yenu yamezingatiwa kwa kadri
ilivyowezekana katika maandalizi tuliyoyafanya ya bajeti hii” Amesema Machela.
Katika Bajeti ya mwaka
2022/2023 , Halmashauri imelenga kutoa vipaumbele vifuatavyo,Makusanyo ya
mapato, elimu , Afya,Usafi wa Mji na utunzaji wa Mazingira, Utawala bora na Mipango Miji.
Post a Comment