Header Ads

DIWANI MAFIGA ATAKA ZOEZI LA USAFI LIWE ENDELEVU

Diwani wa Kata ya Mafiga , Mhe. Thomas Butabile, akifyeka nyasi eneo la shule ya Msingi Mafiga.

Mhe. Butabile akifukua mfereji uliojaa mchanga katika barabara inayopandisha Soko la Manzese.
Diwani wa Kata ya Mafiga, Mhe. Thomas Butabile akiwa na Mtendaji wa Kata ya Mafiga , Kobi Ibrahim katika kukagua maendeleo ya mfaereji unaofukuliwa Soko la Manzese.

DIWANI wa Kata ya Mafiga, Mhe. Thomas Butabile,  ametaka zoezi la usafi liwe endelevu kwa kila Jumamosi wananchi waweze kujumuika pamoja kufaya usafi.

Akizungumza mara baada ya kushiri kufanya usafi katika Jumamosi ya mwisho wa mwezi ,   Mhe. Butabile,  amesema wananchi wajenge tabia ya kufanya usafi kwa hiari ili kuondokana na magonjwa yanayoweza kuzuilika.

Aidha Mh. Butabile ,  amewapongeza waliojitokeza katika zoezi hilo na kuwataka wananchi waendelee na zoezi hilo sio mpaka jumamosi ya mwisho wa mwezi bali usafi uwe ni siku zote katika maeneo yanayowazunguka wananchi  ili kuwasaidia wananchi kuondokana na ujinga pamoja na maradhi yanayowakabili ikiwa ni pamoja na magonjwa ya mlipuko kama Kipindupindu.

"Nataka kila jumamosi kupitia wenye viti wetu na watendaji kwa kushirikiana na wananchi zoezi la usafi lifanyike, maeneo meengi bado machafu sasa sitosikia kwamba mtaa fulani haufanyi usafi hilo halikubaliki, tunataka Kata yetu iwe Kata ya mfano katika Manispaa yetu ya  Morogoro ili iweze kuisaidia Manispaa kuoneaka katika taswira nzuri kwenye suala zima la usafi " Amesema Butabile.

Aidha, ameupongeza Uongozi wa Chama Cha Mapinduzi kwa kujumuika nao katika zoezi la usafi huku akisema ilani inatekelezwa kwa vitendo kupitia viongozi hao.

Katika hatua nyengine, Mhe. Butabile ameshiriki katika zoezi la ufukuaji wa mtaro katika Soko la Manzese ambapo amesema wamechukua hatua hiyo ya kusafisha mtaro baada ya kuona mitaro hiyo imekuwa kero kwa wafanyabiashara .

Amesema kwa kipindi cha muda mrefu mitaro hiyo haikuwa ikifanyiwa usafi hivyo kupitia nguvu za wafanyabiashara na Uongozi wa Kata wameweza kushirikiana vyema kuhakikihsa mitaro hiyo inafukuliwa na inapitisha maji taka kwa urahisi na kuwaondolea kero wafanyabiashara wanaofanya biashara pembezoni mwa mitaro hio.

"Hapa tumeingiza vijana tukiwa tunawalipa fedha ili wafukue hii mitaro, imekuwa kero sana kwa wafanyabiashara wetu jambo ambalo linaweza kuwaletea magonjwa ya milipuko kama vile kipindupindu , hivyo tunaamini mara baada ya kukamilika kwa ufukuaji wa mitaro hii iliyojaa mchanga itapelekea mazingira mazuri kwa wafanyabiashara na barabara inayopandisha kuja soko la Manzese itakuwa rafiki kwa matumizi tofati na ilivyo sasa|" Ameongeza Mhe. Butabile.

Mwisho amewataka wananchi kushirikia katika kuchangia miradi ya maendeleo pamoja na kudumisha  utamaduni wa kuwa wachapa kazi ili kuliendeleza taifa la Tanzania.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.