Header Ads

KERO YA MAJI SHULE YA SEKONDARI MAGOLE YATATULIWA

KERO ya huduma za Maji zilizokuwa zinaikumba Shule ya Sekondari Magole iliyopo jijini Dar es Salaam zimetatuliwa baada ya Shule hiyo kuchimbiwa Kisima kilichogharimu kiasi cha pesa taslimu Milioni Nane na Nusu (Tsh 8,500,000/-) zilizofadhiliwa na Taasisi ya Direct Aid Society.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo wa Maji, Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Omar Kumbilamoto amewataka Wanafunzi wa Shule hiyo kuulinda Mradi huo wa Maji pamoja na kusoma kwa bidii ili kufikia malengo yao katika maisha ya baadae.

Kumbilamoto amesema wataendelea kutatua changamoto nyingine kama upatikanaji wa Walimu wa masomo ya Sayansi ,Viti vya walimu Meza , huku akiwahimiza kusoma kwa bidii na malengo,pia aliwapingeza walimu wanaojitolea ktk kufundisha watoto hao ameahidi kuwa ajira za walimu zitakapotangzwa kipaombelea cha kwanza watawapa walimu wanaojitolea ktk shule hizo za jiji la d.s.m akawahimiza waombe

“Licha ya kupata Kisima, tunajua bado kuna changamoto ya hospital  haijajengwa, kwenye Akaunti ya Kata yenu hii  ya Mzinga  kuna zaidi ya Milioni 180 hazijatumika namuagiza mtendaji wa kata kuharakisha Mchakato wa Manunuzi ili Local fundi apatikane na ujenzi uanze haraka  tutahakikisha kero zote  za matibabu zinatatuliwa kwa Wananchi wote”, amesema Kumbilamoto.


Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Taasisi ya Direct Aid Society, Miraji Mussa amesema wametekeleza mradi huo baada ya kuona changamoto kubwa ya upatikanaji wa Maji katika Shule hiyo, amesema Wanafunzi wanapaswa kuweka sawa na safi mazingira ya Shule yao ili kuvutia zaidi licha ya kuchimbiwa Kisima cha Maji.


Diwani wa Kata ya Mzinga, Job Isaac amewaasa Wanafunzi kusoma kwa bidii, na kumuomba Mstahiki Meya, Kumbilamoto kuhakikisha upatikanaji wa Maabara, Madarasa na Walimu katika Shule hiyo ya Magole.Tukutane Site.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.