Benki ya Taifa ya Biashara NBC imekabidhi mifuko 500 ya seruji kwa Mkoa wa Kigoma kusaidia juhudi za serikali za ujenzi wa madarasa mkoani humo.
Mtendaji wa Mkoa wa Kigoma, Nd Rashid Mchata
akipokea msaada huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Thobias Andengeye pamoja na
kuishukuru Benki ya NBC alisema kuwa kuna uhaba mkubwa wa madarasa kutokana na
muamko wa wazazi wa Kigoma kupeleka watoto shule kufuatia maamuzi ya serikali
kutoa elimu bure.
“Tunategemea wanafunzi wapatao 40,771
kuhitimu darasa la saba na kuingia kidato cha kwanza mwaka 2022 kuepelekea
uhitaji wa madarasa ziaidi ya 1,010 huku mkoa wetu ukiwa na madarasa
405, hivyo mchango wa Benki ya NBC wa mifuko 500 ya saruji utaisaidia kusukuma
malengo serikali yetu ya mkoa kukamilisha ujenzi wa madarasa zaidi ya 605.”
Alisema Nd Mchata.
Akiongea baada ya kukabidhi msaada
huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Nd Theobald Sami alisema kuwa msaada
huo wa mifuko 500 ya seruji yenye thamani ya TSHS 10,500,000 ni kielelezo
kidogo tu cha dhamira ya dhati ya kurudisha kwa jamii kiasi cha faida
inayopatikana kutokana na kuwahudumia Watanzania.
“Sera yetu ya kurudisha sehemu ya faida kwa jamii inayotuzunguka inaangalia maeneo ya elimu, afya na ustawi wa jamii kama nguzo kuu.
Ni kweli mchango wetu huu haitamaliza changamoto ya
vyumba vya madarasa lakini nia yetu kama taasisi ya biashara ni kuendelea
kurudisha sehemu ya faida kwa jamii hivyo tutaendelea kushirikiana na serikali
ya mkoa katika juhudi mbali mbali za kutatua changamoto katika jamii, huu si mwanzo
bali ni muendelezo.” Alisema Nd Theobald Sabi.
Aidha kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Nd Joseph K Rwiza ambaye wilaya yake ni moja kati wa wilaya nufaika wa msaada huo ameishukuru Benki ya NBC kwa mchango wao.
Pia alieleza kwamba serikali ya wilaya yake itaunganisha nguvu za bajeti pamoja
wananchi na wadau wengine kuhakikisha kwamba changamoto ya uhaba wa madarasa
inakuwa historia katika wilaya yake.
Post a Comment