Header Ads

KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU MANISPAA YA MOROGORO YARIDHISHWA NA KASI YA MIRADI YA MAENDELEO.

WAJUMBE  wa Kamati ya Huduma za Uchumi ,Afya na Elimu Manispaa ya  Morogoro , wamefanya ziara ya kukagua miradi ya Maendeleo  huku wakionesha kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa miradi hiyo.

Ziara hiyo imefanyika tarehe 24/1/2025  na kutembelea Shule ya Sekondari ya ghorofa ya Boma B pamoja na  Ujenzi wa Jengo la Utawala na ukarabati wa majengo Shule ya Msingi Mji Mkuu,

Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofautii , wajumbe hao wamepongeza jitihada za serikali katika kihakikisha huduma zinawafikia wananchi wake kwani hatua ya miradi yote ipo hatua nzuri.

sambamba na hayo Wajumbe hao wameagiza Uongozi wa Manispaa kuhakikisha kwamba Shule ya Sekondari ya Ghorofa ya Boma B waalimu kuhakikisha wanatoa ufaulu mzuri kulingana na ubora wa shule hiyo.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kiwanja cha Ndege, Mhe. Majuto Mbuguyu, amewashukuru wajumbe kwa ziara hiyo huku akiwahahakikishia kusimama kidete kuoana miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.

Mhe. Mbuguyu amewapongeza Madiwani wa Kata ya Boma na Mji Mkuu  pamoja na Uongozi wake wa Kata kwa kusimamia vyema miradi hiyo.


Naye, Diwani wa Kata ya Mji Mkuu, Mhe. Hassan Maringo, amesema miradi yote inaendelea vizuri na Uongozi wa Kata ya Mji Mkuu  umekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanasimamia vyema miradi hiyo.


Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Christopher Komba,amesema Manispaa kwa kushirikiana na Menejimenti watahakikisha miradi inatekelezwa kwa kasi na kuendelea kutoa huduma kwa wananchi.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.