KAMATI NDOGO YA MAZINGIRA MANISPAA YA MOROGORO YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA UJENZI WA MITARO YAKUPITISHA MAJI KWENYE MIRADI YA TACTIC
KAMATI ndogo ya Mazingira Manispaa ya Morogoro imeridhishwa na utekelezaji wa ujenzi na uboreshaji wa mitaro ya kupitisha maji machafu kwenye miradi ya Uboreshaji Miji (TACTIC) inayotekelezwa na Manispaa ya Morogoro kupitia ufadhili wa fedha kutoka Benki Kuu ya Dunia.
Kamati hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake, ambaye ni Diwani wa Kata ya Uwanja wa Taifa, Mhe. Rashid Matesa, Januari 20-2025 imefanya ziara na kukagua baadhi ya makaravati pamoja na mifereji inayopitisha maji machafu kwenye miradi ya TACTIC ikiwemo ujenzi wa barabara ya Kihonda Yespa na barabara inayoingia Stendi ya kisasa eneo la Stesheni ya SGR.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Matesa, amesema kamati hiyo imeridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo pamoja na ujenzi wa makaravati ,huku wakiutaka uongozi wa Manispaa ya Morogoro kuendelea kusimamia miundombinu hiyo ili makaravati na mifereji inayotengenezwa isiweze kuleta athari za kimazingira kwa Jamii iliyopitiwa na mifereji hiyo.
Manispaa ya Morogoro ni moja ya Halmashauri ambayo inatekeleza miradi ya TACTIC ikiwa na lengo la kuboresha miundombinu ya miji na kuimarisha utoaji wa huduma kwa jamii.
Manispaa ya Morogoro imepokea Bilioni 19, 606,559.46 kutoka Serikali Kuu kutekeleza miradi ya TACTIC.
Miongoni mwa miradi ya TACTIC ni Ujenzi wa Barabara ya Muhimbili, Tubuyu II, Mjimwema, Barakuda, Kihonda-VETA na Ujenzi wa mifereji ya maji (ANT Mlaria na Kikundi).
Post a Comment