DIWANI MBILINYI AGAWA KADI 54 ZA BIMA ZA AFYA CHF KWA WAZEE KATA YA LUKOBE
DIWANI wa Kata ya Lukobe, Mhe. Selestine Mbilinyi, amewezesha wazee 54 Bima za afya kupitia Mfuko wa Afya ya Jamii(CHF) iliyoboreshwa ambapo lengo lake ni kuona wazee wanaendelea kupata huduma za afya bure.
Kadi hizo amezitoa Januari 21-2025 katika Ukumbi wa JS ikiwa ni ahadi yake aliyoitoa katika sherehe za Baraza la Wazee la Kata ya Lukobe iliyofanyika hivi karibuni Januari 2025.
Akizungumza mara baada ya kugawa Bima hizo, Mh.Mbilinyi amesema kuwa ameamua kufanya hivyo kwa lengo la kutimiza ahadi ikiwa ni pamoja na kutekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi CCM.
“Hii ni awamu ya pili kugawa bima hizi, wazee wetu wametumikia sana hii nchi,malipo ni kuwahakikishia wanapata huduma stahiki ikiwemo hii yz huduma bure ya afya" Amesema Mh. Mbilinyi.
Aidha, Mbilinyi amesema hii ni awamu ya pili kugawa bima hizo kwa Wazee katika kipindi chake cha miaka 5 tangia achaguliwe kuwa Diwani wa Kata ya Lukobe 2020.
Mwisho, Mhe. Mbilinyi amewataka wananchi wa Kata ya Lukobe kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii ili kupata matibabu bure kwani ugonjwa hauna hodi.
Kwa upande wa Katibu Mwenezi wa CCM Kata ya Lukobe, Gassara Zongo, amesema kitendo cha Mh.Mbilinyi kugawa kadi hizo kinawafanya wazee sasa kupata huduma bure na fedha zao ambazo wangetumia katika huduma za afya wanazielekeza kwenye matumizi mengine.
Naye , Katibu wa Baraza la Wazee ,Dr. Bakili Anga, amempongeza Mh. Mbilinyi huku akiwaomba Madiwani wengine pamoja na wadau wa maendeleo kuiga mfano huo ili kuwasaidia wazee katika kuboresha huduma za afya kwa kuwapatia bima za Afya pamoja na mahitaji mengine.
Kwa upande wa Wazee ambao ni wanufaika na bima hizo, Bi. Jamila Murro, akiwawakilisha wazee wenzake wameshukuru jitihada za Diwani Mbilinyi kwa kuwawezesha kujiunga na mifuko ya Bima ya Afya huku wakiwasii viongozi wengine kuiga mfano huo.
Post a Comment