Header Ads

WANANCHI JITOKEZENI KUCHUKUA TEKNOLOJIA ZA KILIMO NA UFUGAJI NANENANE" MD MKONGO

 

Wananchi wa Manispaa ya Morogoro  wametakiwa kufika kwenye maonesho ya Sherehe za Nanenane Kanda ya Mashariki 2024 ili wachukue teknolojia zinazooshwa na wataalam wa kilimo na ufungaji ili kuwawezesha kukima na kufuga kwa tija.


Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro , Emmanuel Mkongo, alipotembelea Mabanda ya Taasisi za umma na binafsi zinazojihusisha na shughuli za Kilimo, Mifugo na uvuvi kwenye viwanja vya Nanenane Kambarage Nyerere Mkoani Morogoro.


"Tumieni siku hizi nane za maonesho haya kuja kuchukua teknolojia kwenye maonesho haya. Mtu akifika hapa ataondoka na kitu, hapa watakuja watu kutoka Mataifa mbali mbali hivyo sisi wenyeji tunapaswa kuwa mstari wa mbele" Amesema Mkongo.

Mkongo, amesema  wakulima na wafugaji wakienda kufanyia kazi teknolojia hiyo hata kwa asilimia 40 tu, wataweza kubadilisha maisha yao pamoja na uchumi na kuifanya Tanzania kuwa Kapu la chakula la Afrika kama ilivyo dhamira ya Mhe. Rais.Dkt. Samia Suluhu Hassan.

"Kiukweli nawashauri wananchi wenzangu waje wajionee mambo mazuri yanayopatikana hapa 88 kwenye mabanda mabalimbali haswa wafugaji wenzangu njooni mjifunze namna ya kufuga kisasa yaani ufugaji wenye tija kwa sababu kunawataalamu wabobezi wa masuala haya watakuelekeza namna bora ya kufuga kisasa na kunufaika na kuacha mazoea ya ufugaji holela usiokuwa na tija" Ameongeza Mkongo.

Kauli Mbiu ya mwaka 2024 ni : “Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”



No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.