Header Ads

WAZIRI MKUU MSTAAFU WA TANZANIA MH.MIZENGO PINDA AITAKA NANENANE KANDA YA MASHARIKI KUTUMIA VEMA FURSA ZA KIUCHUMI ZILIZO KATIKA KANDA HIYO



Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Taznania Mizengo Kayanza Peter Pinda amesema fursa nyingi za kiuchumi zilizopo katika Kanda ya Mashariki ya maonesho ya Nanenane zitasaidia kupiga hatua kubwa kiuchumi endapo zitatumika ipasavyo.


Mizengo Pinda ameyasema hayo Agosti 8,  2024  alipokuwa anafungua rasmi maonesho ya wakulima maarufu kama nanenane kanda ya Mashariki inayoundwa na Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani na wenyeji Morogoro.

Akitoa hotuba yake ya ufungaji mara baada ya kutembelea mabanda ya bidhaa mbalimbali katika Maonesho kwenye viwanja vya vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyoko Nanenane Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Waziri Mkuu amesema Kanda ya Mashariki ina fursa lukuki za kiuchumi na hivyi inaweza kupiga hatua ya haraka kiuchumi.

“sidhani kama kuna Kanda nyingine ambayo iko katika hali nzuri ya kuweza kukua kwa haraka kuliko Kanda ya mashariki, kanda hii ndio inakodolea Mlango wa bandari ya Dar es Salaam” Amesema Mh. Pinda 

Akifafanua zaidi amezitaja fursa hizo kuwa ni pamoja na Bandari za Dar es Salaam na Tanga, uwepo wa ujenzi wa Bomba la mafuta la kutoka Tanga kwenda Uganda, uwepo wa Reli ya mwendo kasi na miundombinu ya barabara za Lami.

Fursa vyingine alizozitaja ni pamoja na uwepo wa vyuo Vikuu vinavyopatikana katika kanda hiyo, kasi ya ukuaji kiviwanda katika Mkoa wa Pwani pamoja na idadi ya wakazi wake wa mikoa hii minne ambao wako zaidi ya milioni 13 sawa na zaidi ya asilimia 21 ya watanzania wote ambao tayari ni soko tosha kwa kanda hii.

Katika hatua nyingine amewataka Viongozi wa Kanda hiyo kuyafanya maonesho ya kanda hiyo kuwa na matokeo kwa wananchi kutokana na maarifa yanayopatikana katika kipindi chote cha maonesho ya nanenane, badala ya kuishia viwanja vya nanenane Morogoro maarifa hayo yashuke kwa wananchi.

Hata hivyo amegusia matumizi ya vyuo vikuu vilivyopo katika Kanda hiyo kikiwemo Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoinne – SUA kupata tafiti zake kuhusu kilimo na kuzitumia badala ya tafiti hizo kubaki kwenye makaratasi.

Kwa upande wake,Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Malima,amesisitiza  suala nzima la kuongeza juhudi ya kuwapa watanzania elimu kuhusu kilimo, kufuga na kuvua kwa kutumia njia bora na za kisasa zaidi.

Aidha, RC Malima,amesema nje  ya kuahidi kutekeleza maagizo aliyoyatoa Mgeni rasmi wakati wa kutembelea mabanda, amewahakikishia wana morogoro na watanzania wote kwa jumla kuutumikia Mkoa huo kwa juhudi zake zote na kwamba matamanio yake ni kuupaisha Mkoa huo.




No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.