Header Ads

NAIBU MEYA MANISPAA YA MOROGORO MHE. CHOMOKA AAHIDI USHIRIKIANO


MADIWANI wa Halmashauri ya Morogoro  wamemthibitisha  Naibu Meya wa Manispaa hiyo, Mhe.Seif Zahoro Chomoka , aliyeshinda kwa kishindo kwa kupata kura zote baada ya Baraza hilo kumthibitisha.

Uthibitishaji wa kumthibitisha Naibu Meya pamoja na kuchagua kamati mbalimbali umefanyika Ukumbi wa Manispaa Agosti 15-2024 katika Baraza la Mwaka la Madiwani la kukamilisha mwaka wa fedha 2024-2025.

Akizungumza mara baada ya uthibitisho wa kuwa Naibu Meya , Mhe. Seif Chomoka, amelipongeza na kulishukuru Baraza kwa kumthibitisha pamioja na kuwapongeza  Wenyeviti Kamati zote waliopita kwakishindo  katika kinyanganyiro hicho ambapo Kamati ya Uchumi na Huduma za Jamii alichaguliwa Mhe. Majuto Mbuguyu, na Kamati ya Mipango Miji na Mazingira alichaguliwa Mhe. Amini Tunda huku Kamati ya Maadili kwa Madiwani ikichukuliwa na Mhe. Thomas Butabile.

Mhe. Chomoka, amelishukuru Baraza la Madiwani kwa kuonesha imani nae, ambapo amewaahidi  madiwani wa Halmashauri hiyo kuwapa ushirikiano na kutetea maslahi ya madiwani wote pamoja na wananchi kwa ujumla.

Aidha, Mhe. Chomoka,amesema  atafanya nao kazi madiwani wote kwa ushirikiano bila kuweka matabaka katika kufanya kazi za chama na Serikali na kuakikisha Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro inasonga mbele katika makusanyo ya Mapato na miradi ya Serikali na kutimiza adhima yake ya kuwa Jiji.

Pia, Mhe. Chomoka,amewapongeza  viongozi wa chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Morogoro Mjini akiwemo  Katibu na Mwenyekiti wake pamoja na mkuu wa Wilaya ya Morogoro  ambapo amesema  yeye ni Mtumishi wa Madiwani wote hivyo atawapa ushirikiano mkubwa.

Mwisho,Mhe. Chomoka,amewaomba  madiwani  waendelee kumuamini katika utekelezaji wa majukumu yake kwani moja ya jukumu kubwa ni kuhakikisha anamsaidia Meya majukumu yake kikamilifu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi na Huduma za Jamii, Mhe.Majuto Mbuguyu,ambaye ni Diwani wa Kata ya Uwanja wa Ndege, amewashukuru Madiwani  kwa umoja wao na kuahidi kushirikiana nao  bega kwa bega ili kuakikisha wanamsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan, Halmashauri hiyo iweze kusonga mbele katika kusimamia miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo sekta ya afya.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, amewapongeza  Wenyeviti Kamati zote waliochaguliwa na kuwataka kufanya kazi pamoja kuakikisha Halmashauri hiyo inafikia malengo yake katika sekta zote .

Mhe. Kihanga, amewataka  madiwani wake kuakikisha wanatoa ushirikiano kwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Ndg. Emmanuel Mkongo  katika ukunyaji Mapato ya Serikali na kusimamia miradi ya maendeleo ndani ya Halmashauri hiyo.

















No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.