ZIARA YA RAIS SAMIA JIMBO LA MOROGORO MJINI YAVUNA WANACHAMA 320 KUTOKA VYAMA VYA UPINZANI,MBUNGE ABOOD AWAPOKEA NA KUWAZINDULIA SHINA LA WAKEREKETWA
ZAIDI ya wanachama 320 wakiwamo waliokuwa wagombea kwa nafasi mbalimbali za Uongozi wa ngazi ya Kata na Serikali za Mitaa Jimbo la Morogoro Mjini kutoka vyama vya upinzani, kikiwamo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na CUF wamejiengua rasmi na kujiunga Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Wanachama hao wamejiunga na CCM kufuatia kumalizika kwa ziara ya kikazi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. samia Suluhu Hassan,ambapo Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Mhe. Dkt.Abdulaaziz Abood, amewapokea leo Agosti 11,2024 na kuwazindulia Shina lao la wakereketwa lililopo Soko la Mawenzi Kata ya Kiwanja Cha Ndege.
Akizungumza leo katika uzinduzi huo wa Shina,Mhe. Abood ,amesema kazi za Rais Samia Suluhu Hassan ndizo zinazovutia wengi kurejea CCM.
Mhe.Abood,amesema ziara aliyofanya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, katika mikoa wa Morogoro hususani Jimbo la Morogoro Mjini imewezesha kuvuna wanachama hao kutoka upinzani kujiunga na chama tawala.
“Tunawashukuru ndugu zetu hawa ambao wameamua kwa hiari yao kujiunga na Chama Cha Mapinduzi na kwa kweli wameingia kwa kishindo maana si kwa wingi huu,” Amesema Mhe.Abood.
''Wana Morogoro bado ninadeni na nyie,naamini kabisa deni hilo nitalilipa, mliitika sana Uwanja wa Jamhuri, hakika mmeiheshimisha Morogoro , umoja wetu uendelee hivi hadi kufikia chaguzi za Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu tupate kura za kishindo " Ameongeza Mhe. Abood.
Akihutubia wanachama waliojitokeza katika uzinduzi wa Shina hilo, Mhe. Abood,amesema , katika miaka mitatu ya Rais Samia, yamefanyika mambo makubwa ambayo hayajawahi kutokea.
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Ndg. Maulid Chambilila, amesem upinzani hawaaminiki wamekuwa watu wa kuzua mambo na uchochezi na hivyo kuwatofautisha kati ya CCM na vyama vya upinzani.
Naye Diwani wa Kata ya Kiwanja Cha Ndege ,Mhe. Majuto Mbuguyu,amesema ataendelea kuwatumikia wananchi wake ili kuendelea kuvuna wanachama wengi zaidi wa vyama vya Upinzani.
Mbuguyu,amemuomba Mbunge kurekebishiwa Soko la Mawenzi pamoja na kuboresha miundombinu ya barabara inayozunguka Soko hilo.
Mwenyekiti wa Shina la Wakereketwa la Walusi Weusi, Hamza Sembeka, amesema amechukua uamuzi huo baada ya kuona juhudi zinazofanywa na Rais Samia, hivyo kumridhisha na kumwahidi Mbunge Abood, kuendelea kuvuna wanachama wengine.
Post a Comment