WENYEVITI WA BODI,WAKUU WASHULE WATAKIWA KUJENGA UELEWA WA PAMOJA JUU YA MPANGO WA SHULE SALAMA
MRATIBU wa Mpango wa Shule Salama kupitia Mradi wa SEQUIP kutoka Ofisi ya Manispaa ya Morogoro,Deogratius Mhaiki,, Mgomapayo ametoa rai kwa walimu wa shule za sekondari waliopatiwa mafunzo ya Programu ya Shule Salama kuhakikisha wanakwenda kuwapa mafunzo walimu wote na wanafunzi katika shule wanazotoka ili kujenga uelewa mmoja wa dhana nzima ya Mpango wa Shule Salama.
Hayo ameyasema Agosti 21-2024 katika uzinduzi wa Mpango wa Shule Salama uliofanyika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Kilakala.
Akizungumza na washiriki wa mafunzo ya utekelezaji wa Mpango wa Shule Salama ,Mhaiki, amesisistiza kuwa walimu hao ni nguzo muhimu katika kuhakikisha wanafunzi wanalindwa dhidi ya vitendo vya ukatili na unyanyasaji na kufanya mazingira yanayowazunguka wanafunzi kubaki salama.
Mhaiki,amesema kila mwalimu kwa kushirikiana na mwanafunzi anapaswa kuwa balozi wa kuboresha mazingira ya elimu kwa kuhakikisha vitendo vyote vya ukatili na unyanyasaji vinadhibitiwa na ili kuwe na mazingira salama ndani na nje ya shule.
Sambamba na hayo, amewaelekeza walimu hao kuzingatia utoaji wa taarifa za utekelezaji wa Mpango wa Shule Salama na utunzaji wa kumbukumbu za kila kinachotekelezwa katika jalada la Mpango wa Shule Salama na kwamba Ofisi ya Rais-TAMISEMI itafanya ufuatiliaji kuona hali ya utekelezaji wa mpango huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Kilakala, Amiri Nondo, amesema Serikali imeanzisha Mpango wa Shule Salama katika shule za sekondari nchini kwa lengo la kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji, pamoja na kuongeza ulinzi na usalama wa watoto.
Nondo,amesema kumekuwepo na changamoto ya mdondoko wa wanafunzi katika shule za msingi na sekondari, jambo linalozuia wanafunzi kufikia malengo ya kielimu ambapo amesema Serikali imechukua hatua mbalimbali kupambana na changamoto hiyo ikiwa ni pamoja na kutoa elimu bila malipo na kujenga shule za sekondari karibu na makazi ya jamii, ili kupunguza umbali wa kufuata shule.
Post a Comment