Header Ads

MAFIGA , TUNGI VINARA MAADHIMISHO YA SIKU YA AFYA NA LISHE MANISPAA YA MOROGORO.


Kata za Mafiga na Tungi, zimeibuka  vinara katika kufanya sherehe za maadhimisho ya siku ya afya na lishe duniani.

Kata hizo zimetajwa Agosti 16-2024 katika kikao Cha kawaida Cha Kamati ya Tathmini ya lishe Manispaa ya Morogoro kikichofanyika Ukumbi wa Manispaa ya Morogoro.

Akizungumza wakati wa ugawaji wa zawadi kwa washindi hao, Mkuu wa Kitengo cha Lishe Manispaa ya Morogoro,Ester Kawishe, amesema Kata hizo zimefanya vizuri sana hususani katika uhamasishaji wa ushiriki wa wanaume kwenye maadhimisho hayo.

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Hilary Sagara, amesema Kata zote ziige Kata hizo mbili katika ushirikishwaji wa wanaume kwenye maadhimisho ya Siku ya Lishe na afya ili elimu ya lishe isambae zaidi kuanzia ngazi ya familia na Jamii kwa ujumla.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.