Header Ads

POCHI LA MAMA LILIVYOKIMBIZA UJENZI WA MADARASA 81 MAPYA MANISPAA YA MOROGORO.

 

HIVI  karibuni Manispaa imepokea tena kiasi cha Shilingi bilioni 1.620,000  kupitia pochi la mama kwa ajili ya  ujenzi wa vyumba vya  madarasa.

Fedha hizo zimetolewa kwa mwezi Septemba kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 81 ya kidato cha kwanza watakaoingia mwakani 2023.

Katika fedha hizo ambazo Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amezitoa kwa ajili ya Ujenzi wa madarasa,, Manispaa ya Morogoro imeunga mkono juhudi za Mhe. Rais kupitia mapato yake ya ndani imeweza kuongeza madarasa 2 na kufanya jumla ya madarasa 83 ambayo asilimia kubwa ya   madarasa pamoja na Meza na viti vimekamilika.

Kwa takwimu hizo, ujenzi wa vyumba vya madarasa 83 vimegharimu kiasi cha shilingi Bilioni 1 na milioni 660.

Hii ni mara ya pili kupokea fedha ,ikumbukwe Manispaa ilipatiwa kiasi cha Shilingi Bilioni 1.7 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 86 ya Uviko 19.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.