Header Ads

KIPIRA AITAKA KAMATI YA ELIMU NA MALEZI KUFANYA KAZI NA WAZAZI KUSIMAMIA WATOTO KIMAADILI NA KUPIGA VITA UKATILI WA KIJINSIA.






MWENYEKITI wa Wazazi CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, CDE. Salum Kipira, ameitaka Kamati ya Elimu na Malezi kwa kushirikiana na Wazazi na walezi  kuwasimamia watoto  katika matumizi ya vifaa vya kielekroniki ili kuwaepusha kujiingiza katika vitendo vya ngono na ukatili mwingine kupitia taarifa zilizopo mitandaoni.

Rai hiyo,ameitoa Desemba 21 , 2022, katika Ukumbi wa Savoy Hotel, katika Mkutano wa Kawaida wa Baraza Kuu la Wazazi Wilaya ya Morogoro Mjini. 

Kipira,amesema katika nyakati hizi, tumeshuhudia watoto wanatumia vifaa ya kielektroniki, ikiwa pamoja na simu na kompyuta kwa lengo la kujifunzia mambo ya masomo, hivyo ni vyema wazazi kuwasimamia watoto wao katika matumizi ya vifaa hivyo, na kuhakikisha wanazingatia matumizi sahihi ya vifaa hivyo ili kuepusha kuanza kuiga na kufanya vitendo vya kikatili.

Amewasisitiza  Kamati ya Elimu na Malezi zifanye kazi sambamba na Idara husika katika Halmashauri pamoja na kushirikiana na Wazazi na Walezi ili kuhakikisha, Usalama wa watoto wakati wote wakiwa nyumbani, katika kipindi hiki pamoja nakuwazuia kwenda kwenye maeneo hatarishi kwa usalama wao kwa kufanyiwa vitendo vya ukatili, ikiwa ni pamoja na kubakwa, kulawitiwa, kushawishiwa kufanya ngono na hata kupata maambukizi ya Corona.

“Katika eneo la malezi ya watoto wetu bado tuna changamoto kubwa ya matumizi ya mitandao, usalama shuleni, kamati zangu fanyieni kazi maeneo haya mkishirikiana na wazazi na walezi ili tuhakikishe tunawasimamia watoto wetu wasijiingize katika masuala yasiyofaa " Amesema Kipira.

Aidha, Kipira, amesema kuwa kumekuwa  na ongezeko la matukio ya vitendo vya ukatili wa kijinsia, hivyo ameziomba kamati husika kutoa elimu ya matukio hayo ili sasa wananchi wengi wapate  uelewa na kuweza kutoa taarifa katika maeneo maalum yaliyoainishwa na  Serikali.

Naye Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa kupitia Wazazi Wilaya ya Morogoro Mjini, Mhe. Hamis Kilongo , amewasisitiza wazazi kuwajibika katika malezi kwa kuhakikisha wanawasimamia watoto wao kwa kufuatilia kwa karibu masuala ambayo yanaweza kusababisha ukatili kwa watoto.

“Wazazi tuwaangalie watoto wetu tusiwaache watoto wakajiamulia baadhi ya vitu ambavyo vitawasababisha waingie katika mambo ambayo yatapelekea kufanyiwa vitendo vya kikatili” Amesema Kilongo.

Hata hivyo, Katibu Elimu na Malezi Wazazi , Godwin Mlambiti, amesema Kamati yake itahakikisha inafanya ziara mbalimbali  kama ilivyoelekezwa ili kupunguza vitendo vya ukatili ikiwa pamoja na utoro, mimba za utotoni ,ulawiti na ubakwaji kwa watoto.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.