Header Ads

KIPIRA APIGA VITA UCHAWA NDANI YA JUMUIYA YA WAZAZI, AWATAKA VIONGOZI KUFANYA KAZI.


  









MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Morogoro Mjini, CDE. Salum Kipira, amesema hataki watu ambao kazi yao ni kujipendekeza ‘chawa’, badala yake anataka viongozi na wanachama wa jumuiya hiyo kuchapa kazi.

Hayo ameyazungumza  Desemba 21 , 2022, katika Ukumbi wa Savoy Hotel, katika Mkutano wa Kawaida wa Baraza Kuu la Wazazi Wilaya ya Morogoro Mjini.

Akizungumza na  Wajumbe wa Baraza hilo, CDE. Kipira,  amesema yeye sio Mwenyekiti wa chawa na kutaka viongozi na wanachama wa jumuiya hiyo kufanya kazi kuanzia ngazi ya Shina, Matawi na Kata, kuangalia malezi ya watoto, maadili na elimu katika shule zinazowazunguka katika Kata zao.

“Leo tumepitisha mpango kazi wa miaka 5, 2022-2027, Tufanye kazi zionekane, jamii ifaidike, tuwe viongozi wenye maadili, viongozi tunapaswa kuwa mfano wa kuigwa, hatuwezi kuwa viongozi ambao hatuna maadili,”Amesema Kipira.

Kufuatia hali hiyo, Kipira  amesema anaandaa mafunzo maalum ya uongozi na kukumbushana misingi ya jumuiya, maadili ya uongozi na malezi yatakayofanyika mwakani 2023.

“Sisi hatuwezi kuwa na kiongozi asiye na maadili, tuwe na uongozi shirikishi sio uongozi wa kimungu, utakachosema ndio hicho hicho hutaki ushauri, hutaki kusikia lolote kwa mtu yoyote, hapana! Uongozi lazima uwe shirikisho,”Ameongeza CDE. Kipira.

Pia katika Mkutano huo, Mwenyekiti alizindua tisheti zitakazovaliwa na Wazazi mwaka 2023 na kuzitaja  Kamati 3 ambazo zilithibitishwa na Wajumbe, miongoni mwa kamati hizo ni Kamati ya Uchumi na Fedha, Kamati ya Elimu na Malezi pamoja na Kamati ya Afya na Mazingira.

Chawa ni msemo ulijichukulia jina katika jamii siku za karibuni, ukimaanisha watu wenye tabia za kumganda mtu mwingine, kujipendekeza na kumsifia kwa nia ya kufaidika naye.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.