MKURUGENZI MANISPAA MOROGORO ATAKA JAMII KUPINGA UKATILI WA AINA ZOTE ILI KUFIKIA MALENGO YA KUWA NA KIZAZI CHENYE USAWA .
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Ally Machela, ameitaka jamii kuhakikisha inapinga ukatili wa aina zote ili kufikia malengo ya kuwa na kizazi chenye usawa kati ya wanawake na wanaume.
Kauli hiyo ameitoa hivi karibuni , ikiwa ni kuelekea kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ambapo kilele chake kitafanyika Desemba 10/2022.
Akizungumza kuelekea kilele cha Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia , Machela, amesema kuwa maswala ya ukatili wa kijinsia yanaleta madhara makubwa katika jamii yasipo shughulikiwa ipasavyo,hivyo kila mwana jamii anawajibu wa kuhakikisha ukatili wa kijinsia unatokomezwa kwa kutoa taarifa kwenye vyombo husika kwa hatua zaidi.
Machela, emesema Manispaa imejipanga kupambana na ukatili wa kijinsia kwa kuanza kupita kwenye mitaa na kata kwa maeneo yote ya Magulio, vituo vya usafiri na nyumba za ibada kwaajili ya kutoa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia.
Katika kuona wanawake wanajikomboa kiuchumi na kuepukana na matendo ya ukatili dhidi yao , amesema kuwa Manispaa ya Morogoro, imeendelea kutenga fedha za asilimia 10 katika mapato yake ya ndani kuwawezesha kiuchumi wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu kwa kutoa mikopo isiyo na riba pamoja na kuwapatia mafunzo ya stadi za biashara kwa wajasiriamali.
Kauli mbiu ya Siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia mwaka 2022 " kila uhai una thamani tokomeza mauaji na ukatili dhidi ya wanawake na watoto’’
Post a Comment