Header Ads

KATIBU UVCCM WILAYA MOROGORO MJINI AWATAKA VIJANA KUJITOKEZA KUWANIA NAFASI ZA UONGOZI.

KATIBU  wa Umoja wa Vijana CCM Wilaya ya Morogoro, Sabrina Juma,  amewataka vijana wa chama hicho kujitokeza kuwania nafasi ya uongozi katika nafasi mbalimbali ndani ya chama.

Kauli hiyo ameitoa leo Julai 04/2022 Ofisini kwake , ikiwa zimepita siku 2 tangia Chama kutangaza nafasi za maombi za kuwania  nafasi mbalimbali.

"Tumeanza mchakato tangia tarehe 02/2022 mchakato wa kuchukua fomu na tutamaliza tarehe 10/7/2022 ambapo huo ndio utakuwa mwisho wa kupokea maombi, niwaombe vijana tujitokeze kuchukua fomu, zoezi linaloendelea  kwa sasa ni uchujaji wa majina ya wagombea nafasi za Kata na leo ndio mwisho, huku tukiendelea na kupokea maombi ya wanaochukua fomu ngazi ya Wilaya " Amesema Sabrina.

Aidha, amesema Vijana ndio chachu kuu ya maendeleo , hivyo kila mwanachama ana haki ya kugombea ili mradi ajue kusoma na kuandika.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.