RC SHIGELA, ANENA MWAKA MMOJA WA RAIS SAMIA SULUHU .
Wajumbe wa kamati ya maandailizi wakishiriki kikao cha Maandalizi ya Maadhimisho ya Maonesho ya Wakulima nanenane yanayotarajiwa kufanyika Agosti 1 mwaka huu Mkoani Morogoro.
MKUU wa Mkoa wa Morogoro,Mhe. Martine Shigela, amemshukuru Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuweza kuwaondolea wananchi wa Mkoa huo kero ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa kipindi hiki kifupi Cha Uongozi wake.
RC Shigela , amesema hayo Julai 2 mwaka huu katika kongamano la wadau wa elimu la kufanya tathmini ya sekta ya Elimu na kumpongeza Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Kiislam cha Morogoro.
Aidha, amebainisha kuwa kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ni cha mafanikio makubwa kwenye Sekta mbalimbali hapa nchini hasa katika Sekta ya maji ambapo zaidi ya shilingi 8bil. zimetumika kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022 katika ujenzi miradi ya kimkakati inayolenga kuwaondolea kero hiyo wananchi wa Mkoa wa Morogoro.
Ameongeza kuwa Miradi ya maji inayotarajiwa kujengwa katika miji 28 nchini kote, Mkoa wa Morogoro ni mnufaika wa mradi mmojawapo utakaotekelezwa Katika Mji Mdogo wa Ifakara ambapo ukamilikaji wake utachangia kwa kiasi kikubwa kukomesha kabisa kero ya Maji kwa wakazi wa maeneo hayo.
“Kwa mwaka wa fedha ulioisha ni zaidi 8Bil. zimetumika katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maji Mkoa mzima kama sehemu ya kusogeza huduma kwa wananchi” amesema Shigela.
“Na zaidi ya Tsh. 50Bil. zimetengwa kuanza kujenga mradi mkubwa wa maji katika Hamashauri ya Mji mdogo wa Ifakara ambapo ni moja ya miradi inaotarajiwa kutekelezwa katika Miji 28 nchi nzima” ameongeza Shigela.
Katika hatua nyingine,RC Shigela, ameweka wazi kuwa kwa upande wa elimu bila malipo Mkoa wa Morogoro kwa kipindi cha mwaka mmoja umepokea zaidi ya 14Bil. kuweza kugharamia elimu bila malipo kwa Shule za Msingi na Sekondari.
Nao wadau wa kada hiyo akiwemo Mwalimu Mipiana Donard Kilasile ambaye ni Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Lukwiva ametoa wito kwa walimu na watendaji wengine kusimamia na kufuatilia vema ufundishaji wa watoto ili kuweza kufikia malengo ya kuinua Mkoa huo kielimu.
Post a Comment