Header Ads

WAKAZI 30 ELFU KUNUFAIKA NA UJENZI WA KITUO CHA AFYA LUKOBE.

Kituo cha Afya Lukobe.




KITUO  cha Afya cha kata ya Lukobe  Manispaa ya Morogoro , kinatarajiwa kukamilika hivi karibuni kitakuwa na uwezo wa kuhudumia zaidi ya Wananchi 30000 na Mitaa  jirani.

Akitoa taarifa ya ujenzi wa kituo hicho  kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi huo  leo Julai 08/2022, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Morogoro, Dkt. Charles Mkumbachepa, amesema kuwa, Kituo hicho kinachogharimu jumla ya sh. Milioni 500 kinajengwa  kupitia fedha za Tozo za huduma za simu ambapo  kikikamilika kitaweza kuhudumia idadi hiyo ya watu na kuboresha huduma za afya.


Aidha, Dkt. Mkumbachepa,ametoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa kuhakikisha Wananchi wa Manispaa ya Morogoro wanapata huduma mbalimbali hususani huduma za afya pamoja na kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Vituo vya afya na Zahanati ambapo kwa Manispaa ya Morogoro wamekamilisha Zahanati 6 na zote zimeanza kufanya kazi.

Mradi huo wa Kituo cha Afya cha Lukobe, ni miongoni mwa miradi itakayopitiwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa  2022 unaoongozwa na Kiongozi wa Mbio hizo 2022 , Ndug. Sahil Geraruma.

Mbali na huduma za afya, Dkt. Mkumbachepa, amewaomba Wananchi wa Manispaa ya Morogoro kushiriki vyema katika SENSA ya Watu na Makazi itakayofanyika mwaka  Agosti 23/2022 ambapo amesema huduma za afya zinazoendelea zitaimarishwa zaidi endapo Serikali watapa idadi nzuri ya Wananchi ili kuoboresha miundombinu na kuwaletea maendeleo.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.