Header Ads

MWAKA 1 WA RAIS SAMIA NA MAFANIKIO MAKUBWA MANISPAA YA MOROGORO.




MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, ameipongeza Serikali ya awamu ya sita,  chini ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, katika jitihada zake cha kipindi cha mwaka mmoja madarakani kwa kufanikiwa kwa kiasi  kikubwa katika kupunguza  changamoto mbalimbali  kwa kuifanya Manispaa hiyo kufanikisha miradi mbalimbali ya Maendeleo.

Kauli hiyo ameitoa Machi 19/2022 katika Kongamano la kuadhimisha mwaka mmoja wa Mhe. Samia Suluhu Hassan lililofanyika  Uwanja wa Jamhuri Morogoro.

Kadhalika, Mhe. Kihanga, amesema Utoaji wa fedha na miongozo ya Mhe. Rais na Serikali yake ya awamu ya  sita imefanya mengi katika Sekta ya elimu ambapo imepunguza sana changamoto za miundombinu ya elimu Sekondari na kufanya upungufu uliokuwepo mkubwa  kupungua sana au kwisha kabisa.

Mhe. Kihanga, amesema katika Sekta ya Elimu Sekondari, Manispaa imepokea fedha za mpango wamaendeleo ya UVIKO-19 jumla ya Tsh.1,720,000,000.00 kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 86 ya Sekondari pamoja na viti 4300 na meza 4300 kwa shule 21 za Serikali ikiwa 17 ni shule zilizokuwepo na 4 zimejengwa mpya.

Aidha, amesema katika fedha hizo za UVIKO-19, jumla ya Madarasa 86 pamoja na viti 4300 na meza 4300 vilikamilika katika muda uliokuwa umetolewa na Serikali.

Hata hivyo, amesema Manispaa kwa kuangalia mtawanyiko wa maeno yake ya kiutawala na kufaulu iliweza kuanzisha ujenzi wa shule mpya 4 za Mazimbu, Tungi, Mbuyuni na Mkundi pamoja na vyoo vya shule zote 4, ambapo hadi sasa shule hizo 4 mpya zimepata usajili na zimefunguliwa na kuanza kutumika na kufanya mradi huo kuweza  kuhakikisha wanafunzi 4300 wa kidato cha kwanza kupata nafasi ya masomo bila adha yoyote.

Pia, amesema , Manispaa ya Morogoro kupitia fedha za mradi toka Serikali Kuu (SEQUIP) chini ya Uongozi wa awamu ya sita tumepokea kiasi cha shilingi Tsh. 940,000,000.00 kati ya 1,200,000,000.00 kwa jili ya ujenzi wa shule mpya nyengine 2 za Mindu na Lukobe kwa lengo la kuboresha miundombinu ya elimu Sekondari ndani ya Manispaa  ambapo ujenzi wa madarasa 16 , maabara 6, maktaba 2, vyumba 2 vya TEHAMA, Majengo 2 ya Utawala na Vyoo matundu 40 na ujenzi unaendeleo vizuri ukiwa hatua za upauaji.

" Manispaa kupitia mapato ya ndani , ndani ya mwaka huu wa fedha 2022/2023 tumeweza  kumalizia maboma 28 ya Sekondari ambayo yalikuwa yameanza kujengwa kwa nguvu za Wananchi  mpaka sasa Manispaa ipo katika hatua za  ujenzi wa shule mpya ya Sayansi -Boma ya Ghorofa yenye madarasa 15 kupitia fedha za mapato ya ndani ambapo jumla ya shilingi Tsh. 684,025,350 zimetumika katika ujenzi huo" Amesema Mhe. Kihanga.

Katika Sekta ya Elimu Msingi, Mhe. Kihanga, amesema Manispaa ya Morogoro ilipokea jumla ya Tsh. 80,000,000.00 fedha za UVIKO-19 kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya ujenzi wa bweni 1 la Watoto 80 wenye mahitaji maalum, ujenzi upo hatua za umaliziaji na umefanyika katika Shule ya Msingi Norto iliyopo Kata ya Kihonda ambapo katika kipindi cha mwaka 1 ,Manispaa  imejenga madarasa 2 kupitia mapato ya ndani.

Upande wa Sekta ya Biashara, Mhe. Kihanga ,amesema ,Manispaa ya Morogoro imeanza kutekeleza mpango wa kuwatoa Machinga barabarani kwa kuwajenga vibanda vya biashara katika maeneo mbalimbali.

Jumla ya vibanda 880 vimejengwa katika eneo la Soko Kuu la Chifu Kingalu Morogoro . Aidha, Manispaa imeanza ujenzi wa vibanda 546 katika maeneo ya faya , mtaa mfupi , masika na Stendi ya Mazimbu ambapo Manispaa imetumia Tsh. 235,000,000.00 fedha za mapato ya ndani kujenga miundombinu hiyo.

Hata hivyo, Manispaa imeishukuru Serikali ya Awamu ya sita chini ya Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa kuipatia Tsh.490,000,000.00 kwa ajili ya kujenga miundombinu ya biashara za Machinga.

Kupitia Sekta ya Afya , Mhe. Kihanga, amesema Manispaa ilipokea jumla ya Tsh. 500,000,000.00 kama fedha za awamu ya kwanza kwa ajili ya Ujenzi wa Hospitali ya Manispaa ,ambapo hadi sasa jumla ya majengo 2 ya OPD na Maabara pamoja na kichomea taka ambapo ujenzi wake upo katika hatua za mwisho za umaliziaji.

Katika Ujenzi wa Kituo cha afya Lukobe, Manispaa ilipokea jumla ya Tsh. 250,000,000.00 kwa ajili ya ujenzi huo, ambapo kwa sasa uujenzi wa Kituo hicho cha afya kipo katika hatua za awali za ujenzi.

Umaliziaji wa Zahanati za Manispaa, Manispaa kupitia fedha za mapato ya ndani inaendelea na mpango wa kumalizia ujenzi wa miundombinu ya afya ya Zahanati 6 ambapo kati ya hizo 2 zimekamilika kabisa na 4 zipo katika hatua za umaliziaji. 

Mhe. Kihanga amesema , Manispaa inategemea kuzifungua ndani ya mwezi wa Aprili 2022, ambapo jumla ya Tsh.300,532,392.00 zimetumika katika ujenzi wa Zahanati hizo.

Sekta ya Mipango Miji, Ardhi na Maliasili, Manispaa ya Morogoro imepokea mkopo wa jumla ya Tsh. 1,000,000,000.00 kutoka Wizara ya ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajili ya kupima Ekari 4500 baada ya Wataalamu kuandika andiko la mradi wa upimaji wa ardhi. Aidha Manispaa imeishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuwezesha kupata fedha hizo na Halamshauri ya Manispaa 


Tutajitahidi kadri iwezekavyo kuhakikisha kuwa shughuli hii ya upimaji  wa Viwanja inakamilika kama ilivyopangwa. Hata hivyo, Manispaa imechangia jumla ya Tsh. 127,600,000.00 kwa ajili ya shughuli ya upimaji kiasi ambacho ni sehemu ya mchango wa Manispaa kwenye mradi wa upimaji wa Viwanja.

Mwisho, Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro inamshukuru Rais wa awamu ya sita Mhe. Samia Suluhu Hasssan kwa jitihada zake katika kuleta maendeleo ya jamii na nchi nzima hususani kwa upendo na uwajibikaji wake katika kuiletea maendeleo Manispaa yetu na kupunguza mrundikano wa wanafunzi uliokuwepo kabla ya yeye kuingia madarakani .



No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.