DC MSANDO AWAONDOA HOFU WANANCHI WA KIEGEA A NA B JUU YA UPIMAJI WA MAENEO.
MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Albert Msando, amewatoa hofu wananchi wa Kiegea A na B Kata ya Mkundi na Kihonda Manispaa ya Morogoro juu ya upimaji wa eneo hilo lenye ekari 4500.
Hayo ameyasema Machi 29/2022 katika kikao juu ya utoaji wa taarifa ya uhakiki na kutangaza zoezi la kupima viwanja katika eneo la mradi la Star City.
DC Msando, amesema katika upangaji na upimaji hakuna mwananchi atakayezurumiwa eneo lake kwani kila mwananchi atapata haki yake kulingana na taaarifa zake za uhakiki zinavyosema.
Aidha, amesema lengo la kupima na kupanga mji huo ni kuona kila mwananchi aliye na kipande anakuwa na hati yake miliki ili kujiletea maendeleo.
"Hatutamuoenea mtu yeyote katika zoezi hili la upimaji, lakini tuwe na huruma sana hatuwezi kuwaachia watu ekari zaidi ya 100 au 50 mtu mmoja kwa ajili ya makazi hii haiwezekani , eneo hili ni kwa ajili ya makazi, biashara na taasisi kwahiyo tunaamini zoezi letu litafanyika kwa umakini mkubwa na kwa ustadi wa hali ya juu'' Amesema DC Msando.
Aidha, DC Msando, amesema kwa sasa Mji unahitaji kupangwa hivyo wananchi lazima wasikilize maalekezo na maagizo ya viongozi badala ya kukiuka maagizo hayo.
"Zipo tabia ambazo viongozi tunatoa maelekezo lakini kuna watu bado wanayapuuza, tabia hiyo siitaki , nataka tukitoa maelekezo tuyafanyie kazi, unazuiwa kuuza na kununua eneno wewe unanunua unataka tukufanyaje? naomba viongozi tusimamie katika hili" Ameongeza DC Msando.
Naye , Afisa Mipango Miji Manispaa ya Morogoro, Emeline Kihunrwa, amesema kwa sasa timu ipo kazini kuhakikisha eneo hilo lote lenye ekari 4500 linapimwa na kupangwa ili wananchi waweze kupata hati zao.
Zoezi la upimaji limeanza Machi 31/2022.
Post a Comment