Header Ads

KONGAMANO LA WANAWAKE MKOA WA MOROGORO LAFANA, RC SHIGELA AWATAKA WANAWAKE KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI

KONGAMANO la wanawake Mkoa wa Morogoro,ambalo liliendana na utoaji hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 631,150,000/=  fedha za Mkopo wa asilimia 10 kwa mwaka wa fedha 2021/2022 Manispaa ya Morogoro,  limefana mkoani humo, ambalo limekutanisha wanawake wa mkoa huo kujadili fursa mbalimbali za kiuchumi na upataji wa haki zao.

Kongamano hilo limefanyika  March 8,2022 Manispaa ya Morogoro katika Uwanjawa Mpira wa Miguu wa  Jamhuri, kwa  kukutanisha wanawake wote wa Mkoa wa Morogoro  ambalo limeandaliwa na Manispaa ya Morogoro kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa .

RC Shigela,  akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo, amesema wanawake ni kundi kubwa katika kuleta maendeleo ndani ya jamii na Taifa kwa ujumla, hivyo kupitia jukwaa hilo zipo fusra  mbalimbali za kiuchumi zilijadiliwa ambazo zipo mkoa wa Morogoro  pamoja na kubadilishana uzoefu wa kibiashara.

Aidha, RC Shigela, amesema kuwa Mkoa wa Morogoro, una fursa nyingi za kiuchumi zikiwamo za madini na kilimo, lakini fursa hizo kwa upande wa wanawake kiuchumi zimekuwa zikiwekwa pembeni na kunyimwa haki zao.

"Kupitia Kongamano hili la wanawake, natarajia mpate mtandao wa kufanya biashara na kukua kiuchumi, nawapenda sana wanawake, na wala sijawahi kugombana na wanawake, kwa kipindi changu cha Uongozi  nataka niache alama hapa Morogoro  kuwepo na idadi kubwa ya wanawake ambao ni matajiri na wenye kumilika mali mbalimbali," Amesema Shigela.

Aidha, RC Shigela,  amesema ingependeza kwa kila Wilaya kuweka mikakati ya kuandaa makongamano ya wanawake kila baada ya miezi mitatu, ili waendelee kujadili mambo mbalimbali, zikiwamo fursa za kiuchumi na kupata haki zao.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro, Bi. Doroth Mwamsiku, amewataka Wanawake  kuendelea kuunga mkono  juhudi za Rais Samia Suluhu Hassani katika masuala ya kimaendeleo na kiuchumi, kama kauli mbiu ya Kongamano hilo inavyosema "KIZAZI CHA HAKI NA USAWA KWA MAENDELEO ENDELEVU".

Mwamsiku, amewataka wanawake Mkoa wa Morogoro , kuvunja ukimya juu ya vitendo ya ukatili wa kijinsia ambavyo wamekuwa wakifanyiwa, na kuacha kukaa na maumivu hayo na hata kuwasababishia ulemavu na vifo, bali wapaze sauti kufichua vitendo hivyo na kuishi salama.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Albert Msando,amesema  malengo mahususi ya Kongamano hilo la wanawake, ni kufahamiana, kubadilishana mawazo pamoja na kujenga mtandao wa kibiashara na kuinuana kiuchumi.

"Nawapongeza pia wanawake wa mkoa wa Morogoro  kwa kujituma kufanya shughuli mbalimbali, ambapo tangu nifike hapa Morogoro nimeona wanawake wengi wakijishughulisha, hivyo natoa wito kwa wanawake msikae bila kufanya kazi fursa zipo nyingi zitumie kujikwamua kiuchumi," Amesema DC Msando.

Nao baadhi ya wanawake wamempongeza Mkuu huyo wa Mkoa wa Morogoro ,kwa kushiriki katika  Kongamano hilo, ambalo limewafumbua na kubadilisha uzoefu wa kibiashara na kuinuka kiuchumi.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.