DC MSANDO APIGA MARUFUKU SAFARI KWA WASIMAMIZI WA UJENZI WA MADARASA 86 YA UVICO-19.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Albert Msando, akizungumza na Madiwani katika Baraza Maalum la kupitia taarifa ya mkakati wa Ujenzi wa Madarasa mapya 86 kutoka katika fedha za ujenzi wa miundombinu ya mpango wa Maendeleo kwa ustawi wa Taifa dhidi ya UVICO-19.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga (kulia) akipitia jambo na Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Ally Machela.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Albert Msando, amepiga marufuku watumishi wanaohusika na miradi ya UVICO-19 kutosafiri kwa muda ambao ujenzi wa miradi hiyo ya shule ikiendelea ili kusimamia miradi hiyo kwenye maeneo yao.
DC Msando, ameweka zuio hilo hivi karibuni ,alipokuwa anazungumza na Watumishi pamoja na Madiwani katika, Baraza Maalum la Madiwani la kupitia maelekezo ya mkakati wa Ujenzi wa Madarasa mapya 86 kutoka katika fedha za ujenzi wa miundombinu ya mpango wa Maendeleo kwa ustawi wa Taifa dhidi ya UVICO-19.
Aidha , DC Msando, amesema kuwa amechukua uamuzi huo kufuatia kuingia kwa fedha ya ujenzi wa Madarasa mapya 86 kutoka katika fedha za ujenzi wa miundombinu ya mpango wa Maendeleo kwa ustawi wa Taifa dhidi ya UVICO-19 ambayo ukamilishaji wake unatakiwa hadi kufikia Desemab 15 madarasa hayo yawe yameshakamilika ili wanafunzi waingie darasanai mwakani.
Hata hivyo, amesema kuwa kutokana na majukumu hayo, amelazimika kuzuia watumishi wote wanaohusika moja kwa moja na shughuli za mradi wa madarasa kuto safiri kwa muda hadi pale madarasa hayo yataka[okamilika.
“Kuanzia leo nazuia safari zote zisizo za lazima kwa watumishi na watendaji wanaouhusika na ujenzi wa madarasa haya ya UVICO-19, hadi pale madarasa haya yatakapo kamilika, hii sio pesa ya kuweza kuwanufaisha na kuwafurahisha watu, Mhe. Rais ametoa fedha kwa ajili ya mkakati maalumu wa kuwasaidia watoto wetu , hatutaki tumkwamishe tufanye kazi na tuvumiliane lengo ni kuona madarasa yanakamilika na watoto wetu mwakani waingie katika madarasa hayo " Amesema DC Msando.
Pia, ametaka madarasa hayo mara baada ya kukamilika yaoneshe thamani ya fedha pamoja na ubora na sio yamekamilika yakawa na dosari.
" Hata hivyo, nataka vifaa vyote vya manunuzi vinunuliwe kwa mzalishaji na sio mtu wa kati, na sitegemei kama tutaenda kwa mtu wa kati, nataka kuona kamati zinaundwa ikiwemo kamati ya ufuatiliaji na utekelezaji wa mradi, na utekelezwaji huu unapaswa kuanza ndani ya wiki 2 baada ya kuingia kwa fedha hizo na mradi huu wa madarasa lazima ukamilike ifikapo Desemba 15/2021 kwani pesa tayari zimeingai kauznia Oktoba 18/2021 zina wiki ya pili sasa lakini pia sitegemei kuona mabadiliko ya mradi maana muda wa kuwasilisha mabadiliko ya mradi ulishaisha " Ameongeza DC Msando.
Mwisho, amewataka Madiwani wakiona kuna ubabaifu wa kuwatafuta wadhabuni kujenga madarasa hayo , basi mradi huo waupeleke moja kwa moja kwa Jeshi la Magereza badala ya kuendelea kusigana na kusababisha kutofikia lengo la fedha hizo.
Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, amewataka Madiwani wasimamie kikamilifu miradi hiyo ili kusijitokeze dosari katika ujenzi wa madarasa yanayotajaiwa kuanza kujengwa mapema mwa juma hili.
." Niwatoe hofu wataalamu, Chama na Mkuu wa Wilaya, sisi tumejipanga kuona tunapita Kata kwa Kata kuoona jinsi ujenzi wa madarasa unavyoendelea, lengo ni kuona pale wanapokwama ili sisi tuweze kukwamua, hatutarajii kuona madarasa yamekamilika ndipo dosari zionekane , kila Diwani atengeneze timu yake na kujiwekea utaratibu wa kukagua ujenzi wa Madarasa katika Kata yake" Amesema Mhe. Kihanga.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Ally Machela, amesema mwaka huu 2021 Manispaa ya Morogoro inatarajia kufungua shule 7 mpya za Sekondari.
Katika ukamilishaji wa madarasa ya UVICO-19, Machela, amesema wamejipanga kufanya ufuatiliaji na usimamizi wa aina mbili ikiwamo ya kwanza ya kutembea na madiwani wote kukagua ujenzi huo baada ya ujenzi kuanza na awamu ya pili ujenzi ukiwa unaendelea kuwa mwishoni kupitia Baraza la Madiwani ili na wao waweze kushauri kwa pamoja na kuwa na madarasa bora.
" Manispaa tumejipanga kuhakikisha madarasa haya yanakamilka kwa wakati, lakini pia katika kuona shule hizi waalimu wake wanakuwa katika mazingira rafiki, tumejipanga pia kujenga Majengo ya Utawala katika shule 8 hadi 10 mwaka ujao wa fedha 2022/2023 ili majengo yanayotumika kama Ofisi yarudi kutumika na wanafunzi " Amesema Machela.
Post a Comment