KAMATI YA FEDHA MANISPAA YA MOROGORO YATOA MAELEKEZO HAYA UJENZI WA MADARASA KUPITIA FEDHA ZA UVICO-19.
Jengo la Hospitali ya Manispaa ya Morogoro.
Jengo la Hospitali ya Manispaa ya Morogoro.
KAMATI ya Fedha Manispaa ya Morogoro leo imetoa maelekezo katika ziara ya kukagua hatua za ujenzi wa Madarasa katika shule za Sekondari, zilizopokea fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa kupitia fedha za Uviko-19.
Katika ukaguzi huo, Kamati ya fedha ilitoa maelekezo katika kuzijengea uwezo kamati za ujenzi za shule ili waweze kutekeleza miradi hiyo kwa ufanisi.
Kamati hiyo ya fedha, imezitaka kamati za ujenzi kuijulisha jamii/wananchi juu ya neema ya serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na na Rais Samia Suluhu Hassan kwa wananchi wao kuhusu fedha hizo za mradi.
Mwisho, Kamati hiyo, iliwasisitiza wajenzi kuzingatia vipimo vyote vinavyotakiwa kufanyika kufuatwa ikiwa ni pamoja na kina cha msingi na uwiano wa mchanga na saruji kuzingatiwa.
Miongoni mwa Shule zilizotembelewa na Kamati hiyo ni pamoja na Shule Mpya ya Sekondari Mkundi, Shule ya Sekondari Kola Hill, Shule ya Sekondari Kingo, Shule ya Sekondari Bondwa pamoja na Shule ya Sekondari Mafiga.
Kupitia fedha za UVICO-19, Manispaa ya Morogoro imepata fedha zitakazoweza kujenga Jumla ya Madarasa mapya 86 ili kupunguza Msongamano darasani katika kujikinga na Ugonjwa wa Corona.
Licha ya kukagua ujenzi wa madarasa, Kamati ilitembelea na kukagua ujenzi wa Hospitali ya Manispaa na kuridhika na kasi ya ujenzi huo.
Post a Comment