DIWANI KATA YA MZINGA AWAPONGEZA WANANCHI KUSHIRIKI UJENZI WA SHULE MPYA YA SEKONDARI.
DIWANI wa Kata ya Mzinga, Mhe. Salumu Chunga, amewapongeza Wananchi wa Kata ya Mzinga kwa kujitoa kwao katika kufanikisha zoezi la kuanza ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari.
Pongezi hizo, amezitoa Novemba 22/2021, katika zoezi la kuangusha miti mikubwa na vichaka katika eneo linalotarajiwa kujengwa shule hiyo.
Mhe. Chunga, amesema ujenzi wa shule hiyo mpya ya Sekondari itapunguza changamoto katika Sekta ya Elimu kwenye Kata hiyo.
Aidha, Mhe. Chunga, amesema kuwa ushirikiano uliooneshwa na wananchi wa Kata hiyo katika ujenzi wa shule ya Msingi Konga ndio ushiriikiano unaotakiwa kufanyika katika ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari kwani uwepo wa shule hiyo ya Sekondari katika Kata hiyo utaleta manufaa katika jamii na kufanya Wanafunzi wasome karibu na nyumbani na kuacha kusafiri umbali mrefu.
Hata hivyo, Mhe. Chunga, amewashukuru wananchi kwa kujitoa kwaajili ya maandalizi ya ujenzi huo kuwaahidi kuwa ataendelea kuwashirikisha wadau wengine watakaosaidia kuongeza nguvu kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi wa Shule hiyo.
"Tunaamini mradi huu utakapokamilika utatatua changamoto zilizopo katika Sekta ya Elimu katika Kata yetu ya Mzinga, na kufanya wanafunzi kupata Elimu kwa urahisi kwani kwasasa hutembea umbali mrefu kwenda shuleni, ujenzi wetu tutaanza na vyumba 3 vya madarasa kwa nguvu za Wananchi kisha tutaendelea na ujenzi kadri tutakapojaliwa nguvu ili kufanikisha ndoto ya kuwa na Shule yetu ya Kata "Amesema Mhe. Chunga.
Mwisho, Mhe. Chunga, kuwa moja ya tatizo la watoto wao kushindwa kufanya vizuri kitaaluma ni umbali wa shule ambazo wanasoma hivyo amewaomba Wananchi kuongeza nguvu pamoja na Serikali li kuepukana na changamoto hiyo.
Post a Comment