RC SHIGELA APIGA MARUFUKU MICHANGO ISIYO NA KIBALI MAALUM SHULENI.
MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Martine Shigela, amepiga marufuku michango ya Shuleni bila kibali cha Serikali pamoja na ‘Tution’.
RC Shigela, ameyasema hayo katika ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Madarasa ya mpango wa UVICO-19 kupitia fedha zilizotolewa na Serikali kufanikisha ujenzi wa Madarasa hayo katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.
“Nina agiza katika mkoa wangu wa Morogoro marufuku michango na tuisheni shuleni bila kibali tutekeleze mpango wa elimu bila malipo bila kuwachaji wananchi, niwaambie tu Wazazi, tulipokea Waraka wa Serikali Elimu bila malipo hivyo walimu marufuku kuwachangisha pesa za tuisheni Wazazi" Amesema RC Shigela.
Katika ziara hiyo, RC Shigela, aliambatana na wakuu wa Idara wote na Wataalam wote katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro pamoja na Wakuu wa Taasisi za Serikali kama vile MORUWASA, TANESCO, FIRE, JESHI LA POLISI, huku baadhi ya mashauri yalitatuliwa hapo hapo mengine aliyaelekeza katika mamlaka husika.
Post a Comment