Header Ads

NAIBU MEYA MANISPAA YA MOROGORO, AWATAKA WAZAZI KUWEKEZA KATIKA ELIMU.

 

Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Mohamed Lukwele,  akimkabidhi cheti muhitimu.(kushoto) Mkurugenzi na Mmiliki wa Shule ya Patricia na Diwani wa Kata ya Mafiga,Mhe. Selestine Mbilinyi.

Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Mohamed Lukwele, (watatu kutoka kulia), Mkurugenzi na Mmiliki wa Shule ya Patricia na Diwani wa Kata ya Mafiga,Mhe. Selestine Mbilinyi (wapili kulia) wakiambatana na Viongozi wa Serikali za Mitaa pamoja na Waalimu wa Patricia katika picha ya pamoja ya wanafunzi waliobeba picha za Marais 6.

      

      

      

Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Mohamed Lukwele, akizungumza na Wazazi katika Mahafali.

Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Mohamed Lukwele, (katikati) akisindikizwa na Skauti kuingia Uwanjani.
Mwanafunzi akionesha uwezo wa kuimba Uwanjani.
                
Mwalimu akiwa na wanafunzi wake.
               
Wahitimu wakionesha uwezo wa kuimba na kucheza mbele ya Mgenio rasm,  Mhe. Mohamed Lukwele.

           
Wananchi  na wazazi waliohudhuria katika Mahafali.

NAIBU Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Mohamed Lukwelee ,amewataka Wazazi  pamoja na wananchi wa Manispaa ya Morogoro   kuwekeza katika elimu kwa kuwapeleka watoto wanaotakiwa kuanza shule na kuondokana na janga la kukosa elimu.

Kauli hiyo, ameitoa  leo Desemba 08/2021  , wakati akizungumza na Wazazi pamoja na wageni waalikwa waliohudhuria katika Mahafali ya 3 kwa darasa la awali Shule ya awali na Msingi ya Patricia iliyopo Kata ya Lukobe ambapo Mhe. Lukwele alikuwa Mgeni rasmi katika Mahafali hayo.

Akizungumza na Wazazi wa wanafunzi pamoja na wananchi waliojitokeza katika Mahafali hayo, Mhe. Lukwele, amesisitiza  umuhimu wa wazazi kuwaelimisha na kuwapatia elimu watoto wao.
  
Amesema kuwa,  maendeleo miongoni mwa jamii yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na kiwango cha uwekezaji katika elimu, ni vema jamii iwekeze kwa kiwango kikubwa katika sekta ya elimu ili kujikwamua na umaskini uliopo na kupambana katika soko la ajira.

 "Wazazi tuwasimamia watoto wafikishe ndoto zao na hakuna urithi mzuri kwa mtoto kama elimu, tukiwapeleka shule watakwenda kufanya kwa bidii, kusoma kwa bidii ili wawe na vipato vyao kuliko tegemezi tupeleke watoto shule na wao wakawe watu wazuri kulijenga Taifa lakini tuwafundishe uzalendo na utamaduni tutie msukumo mkubwa kwenye elimu tuwasimamie na kuwaombea maana bila Mwenyezi Mungu  hakuna jambo litakalo kwenda vizuri " Amesema Mhe. Lukwele.


“Tukumbuke kwamba kuwekeza katika elimu ni mkakati wa muda mrefu unaohitaji dhamira, subira na kwamba matokeo yake huonekana baada ya muda mrefu wa uwekezaji na faida kwa wazazi mara baada ya mtoto kusoma na kuweza kumsaidia pindi azeekapo” Ameongeza Mhe. Lukwele.

Hata hivyo, Mhe. Lukwele, amesema  wazazi ambao wanashindwa kuwekeza katika elimu na kuwafanya watoto wao kudhurura mitaani na kuwajengea ugumu wa maisha watoto hao bila kuwa na elimu na kuwataka kukazania elimu kwa watoto wao kwanza.
 
Aidha, Lukwale, amesema Manispaa ya Morogoro hususani Kata ya Lukobe, na rasilimali nyingi zinazohitaji viongozi wabunifu watakaohakikisha zinatumiwa vizuri kwa faida ya watu wote hivyo bila kuwekeza katika elimu rasimali hizo zitatumiwa vibaya na watu wasiojua faida ya elimu.

Mara baada ya kuzungumza na Wazazi, Mhe. Lukwele, alipata nafasi ya kugawa vyeti kwa Wahitimu pamoja na zawadi kwa waliofanya vizuri katika masomo yao na kuahidi kuchangia  Mabati 30 katika kufanikisha ujenzi wa Bwalo na Bweni la wanafunzi wa shule hiyo ya Patricia.
 
Kwa upande wa Mkurugenzi ambaye pia ni Mmiliki wa Shule ya Patricia Pre & Primary  na Diwani wa Kata ya Lukobe, Mhe. Selestine  Mbilinyi, amesema katika kuhakikisha Kata ya Lukobe anaipeleka kwenye  kilele cha mafanikio, atahakikisha barabara zinazotakiwa kuiunganisha Kata hiyo ya Lukobe na Mitaa Mingene  zaidi zinajengwa. 

Amesema kuwa, hatua hiyo ya kuunganisha Mitaa kwa ujenzi wa Vivuko kutoka Mtaa mmoja kwenda Mtaa mwengine itaongeza shughuli za uwekezaji, kilimo na biashara na hivyo kuwaongezea kipato wananchi wake.

Mwisho, Mh. Mbilinyi , amempongeza Naibu Meya kwa ushiriki wake katika sherehe hiyo ya kuhitimu kwa darasa la awali wanaojiandaa kuingia darasa la kwanza mwakani 2022 na kuwaomba Wazazi kuendelea kushirikiana na Walimu katika suala la makuzi na malezi ya Watoto.


Katika Mhafali hayo, ilishuhudiwa michezo mbalimbali iliyooneshwa na Wanafunzi hao ikiwamo sanaa ya maonesho ya michezo kwa  Skauti, Uchezaji wa Dansi kwa wanafunzi, Uimbaji, maonesho ya kuzungumza lugha ya Kichina na tafsiri yake, vipaji vya utangazaji wa habari pamoja na kusikiliza nyimbo ya pamoja ya shule yao waliyoaandaa wanafunzi katika Mahafali hiyo.



No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.