Header Ads

TIMU YA MADAKTARI BINGWA 49 WA RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN YAPIGA KAMBI YA SIKU 8 MKOA WA MOROGORO KUENDELEA NA KAMPENI YA KUTOA HUDUMA KWA WANANCHI


KATIKA kuendelea kuboresha huduma za afya nchini, Timu ya Madaktari Bingwa wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wameibukia Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kutoa huduma ya afya kwa siku 8  katika Halmashauri zote za Mkoa wa Morogoro kuanzia Juni 9- 16 hadi 20 Mwaka 2025.

Kauli hiyo imetolewa Juni 9-2025 katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro, Herman Tesha , wakati akizungumza na Madaktari hao watakao toa huduma za kibingwa na bobezi katika Mkoa wa Morogoro 

Aidha, Tesha,amesema kambi hiyo pia italenga zaidi  kuwajengea uwezo wataalamu wa afya waliopo katika hospitali zilizopo katika Halmashauri hizo.

Hata hivyo,Tesha,  amewasisitiza Madaktari hao kutoa hamasa kwa wananchi kuwa na utamaduni wa kupima afya mara kwa mara ili kujua hali za afya zao  kwani itasaidia wananchi kujitambua mapema hasa kwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza na kuanza uchunguzi mapema ili kuanza matibabu mapema.

" Nawashukuru sana Madaktari bingwa ,pamoja na Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwaleta katika awamu nyengine mkoani kwetu, kwani huduma ya afya mtakayokwenda kutoa kwenye Halmashauri zetu ni huduma muhimu sana kwa Jamii nendeni mkawasaidie wananchi" Amesema Tesha.


Kwa upande wa Mratibu wa Kambi ya Madaktari Bingwa Mkoa wa Morogoro, Jackline Ndanshau,  amesema Kambi hiyo ina jumla ya Madaktari Bingwa 49 ambapo watatoa huduma hizo za kitabibu katika Mkoa wa Morogoro kwa siku 8 na wananchi zaidi ya 3000 watanufaika na Kambi hiyo.

Ndanshau, amesema Kambi hiyo ya madaktari bingwa,italenga zaidi pia kutoa  uzoefu kwa jumla ya wataalamu wa afya 200 katika upande wa magonjwa ya wakina mama, watoto,ukunga, pamoja na huduma za upasuaji.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Dkt. Best Magoma,amesema wamepokea ugeni huo watatoa ushirikiano wa hali ya juu ili adhima ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutoa huduma bora kwa wananchi ikamilike.

Dkt.Magoma,amewataka wataalamu wa afya katika Halmashauri ambazo zitakuwa na madaktari bingwa kutumia fursa hiyo kujiongezea uzoefu wa kitatbibu.

Miongoni mwa Madaktari Bingwa wa upasuaji kutoka Hospiatali ya Benjamini Mkapa Dodoma,Dkt. Costantine Yamoyoni,amesema watatumia siku 8 za kambi kutoa huduma bora kama malengo ya Kampeni hiyo yanavyotaka ili kutimiza ndoto ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwahudumia wananchi kuwa na afya bora katika ujenzi wa Taifa.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.