Header Ads

MBILINYI AWATAKA WANAFUNZI WA SEKONDARI TUSHIKAMANE KUSOMA KWA BIDII ILI KUFIKIA MALENGO



WANAFUNZI Shule ya Sekondari Tushikamane Manispaa ya Morogoro,  wametakiwa kusoma kwa bidii na kufanya vizuri katika mitiani yao ya mwisho pasipo kusikiliza vishawishi vya wazazi vinavyowataka wafanye vibaya kwenye mitihani ili wakawasaidie shufguli zao mbalimbali.

Hayo ameyasema Diwani wa Kata ya Lukobe Mhe.Selestine Mbilinyi akiwa mgeni rasmi ,  katika Mahafali ya Shule hiyo yaliyofanyika Ukumbi wa Iswilo Manyuki Novemba 3-2024.

Mbilinyi, amesema baadhi ya wazazi wamekuwa wakiwaambia watoto kuwa wasifanye vizuri katika mitihani yao ya mwisho kwa kukwepa majukumu yao ya kuwaendeleza kitu ambacho  kinarudisha Maendeleo ya elimu.

“Ninawaasa msome kwa bidii ili muweze kufikia malengo yenu mnapaswa kuwasikiliza wazazi wenu kwa mambo mazuri watakayokuwa wanawashauri, lakini endapo watawashauri mfanye vibaya kwenye mitihani yenu ya mwisho ili kukwepa gharama ya kuwaendeleza kwa madai kuwa watawapeleka kusomea ufundi na wengine wakidai kuwa mkawasaidie shughuli za shamba,biashara  msikubali maana wanakatisha ndoto zenu”, Amesema Mbilinyi

Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari Tushikamane, Mwal.Samulek Kundayo, amesema wamejipanga vizuri kwa kushirikiana na waalimu wake kuhakikisha wanafunzi wanafaulu mitihani yao.

Kidato cha Nne wanatarajiwa kufanya mitihano yao ya Taifa Novemba 11-2024.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.