DC KILAKALA AHIMIZA WANANCHI WA WILAYA YA MOROGORO KUJITOKEZA KUPIGA KURA UCHAGUZI
MKUU wa Wilaya ya Morogoro amewahimiza wananchi waliojindikisha kwenye daftari la mkaazi wametakiwa kwenda kupiga kura ifikapo Novemba 27-2024 ili kuwapata viongozi bora watakao waletea maendeleo katika maeneo yao.
Kauli hiyo ameitoa Novemba 16-2024 mara baada ya kumalizika kwa mbio fupi zilizoshirikisha wanamichezo mbalimbali, watumishi wa taasisi za Umma , binafsi na Serikali zikilenga kuhamasisha wananchi kupiga kura.
DC Kilakala, amesema mfumo wa nchi ni wakidemokrasia hivyo lazima wananchi wapige kura ili kuwapata viongozi bora.
Aidha, DC Kilakala, amesema ni haki kwa kila aliyejiandikisha katika daftari la mkaazi kutumia fursa hiyo kwenda kupiga kura wakati utakapofika.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro ambaye ndiye Msimamizi wa Uchaguzi, Emmanuel Mkongo,amesema maandalizi yanaenda vizuri ili kufanikisha uwe wa huru na haki.
"Maandalizi yanakwenda vizuri sana, tayari mchakato wa kusikiliza rufaa umekamilika na sasa kilichobakia ni mchakato wa maandalizi ya kampeni, naamini wasimamizi wa ngazi ya Kata na Mitaa wamepata mafunzo mazuri na watasimamia vyema mchakato mzima wa uchaguzi ili kuepuka changamoto zinazoweza kujitokeza" Amesema MD Mkongo.
Pia ,Mkongo amewashukuru wananchi wa Manispaa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwa asilimia 110 na kuvuka lengo.
Nao baadhi ya wananchi wa Manispaa ya Morogoro wamesema wako tayari kupiga kura na kuchagua viongozi ambao watasimamia vyema shughuli za maendeleo na kutatua changamoto zinazoikabili jamii.
Post a Comment