DC KILAKALA AWAKUTANISHA WADAU WA MAENDELEO KUTATUA CHANGAMOTO YA MADAWATI SHULENI
MKUU wa Wilaya ya Morogoro,Mhe. Mussa Kilakala, amewakutanisha wadau wa maendeleo kutoka Taasisi mbalimbali pamoja na mashirika binafsi kwa lengo la kuchangia na kutatua tatizo la madawati na changamoto za elimu katika Wilaya ya Morogoro.
Kikao hicho cha wadau wa maendeleo kimefanyika katika ukumbi wa Mikutano Ofisi Kuu ya Manispaa Novemba 18-2024.
Akizungumza na wadau hao, DC Kilakala amesema Wilaya ya Morogoro kupitia Halmashauri zote mbili Manispaa ya Morogoro na Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro zinakabiriwa na tatizo la rasimali fedha katika utengenezaji wa madawati .
Aidha,DC Kilakala,amesema wadau hao kukutana anaamini watalibeba suala hilo kama ajenda nyeti kwao ili kushirikiana na Serikali katika kutatua tatizo la madawati,viti na Meza na kuwafanya wanafunzi kusoma katika mazingira rafiki yatakayomfanya aweze kufanya vizuri katika masomo yake.
"Nimewakutanisha wadau wetu wa maendeleo, katika Wilaya yetu tuna tatizo kubwa la madawati,viti na meza,kuwaita hapa ni kuwashirikisha changamoto yetu, kuwaambia hali halisi ya elimu yetu, naamini tutafika sehemu ambayo itakuwa na unafuu kama wadau hawa watabeba ajenda hii na kuiona ina umuhimu sana katika kukuza sekta ya elimu ndani ya Wilaya yetu pamoja na kuwatengenezea wanafunzi mazingira mazuri ya kusomea ili kukuza ufaulu wa wanafunzi" Amesema DC Kilakala.
Post a Comment