MANISPAA YA MOROGORO YAANZA ZOEZI LA UUZAJI VIWANJA , RC MWASA ATOA KAULI NZITO KWA VISHOKA.
WAKATI Manispaa ya Morogoro ikianza rasmi zoezi la uuzwaji wa Viwanja eneo la Kiegea A na B Star City mara baada ya kumalizika kwa mgogoro uliodumu kwa muda mrefu, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwassa, amepiga marufuku madalali wa uuzwaji wa Viwanja (Vishoka) ambao wamekuwa vyanzo vya migogoro ya ardhi.
Kauli hiyo
ya Mkuu wa Mkoa, ameitoa Novemba 30/2022 wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa
mpango wa kutangaza na kukabidhi Viwanja
vilivyopimwa na Manispaa ya Morogoro eneo la Star City Kiegea.
Akizungumza
katika uzinduzi huo, RC Mwassa, amewataka wananchi watakaopewa fidia na wale
watakaonunua Viwanja marufuku kuuza kiholela Viwanja hivyo kwani kufanya hivyo
kunasababisha migogoro ya ardhi.
Aidha, RC
Mwassa, amesema mwananchi yeyote atakayetaka kuuza Viwanja vyake lazima
awasilishe maombi kwa Mkurugenzi wa Manispaa ikiwa imeonyesha orodha ya Viwanja
anavyokusudia kuviuza.
“Migogoro
imeisha, wale mabingwa wa kuuza viwanja bila kufuata utarartibu iwe mwanzo na
mwisho, vishoka nitakula naoa sahani moja,lazima madalali wa viwanja tuwaondoe,
haiwezekani tumetumia nguvu kubwa ya kutatua mgogoro wao waanziishe upya hili
sitalivumilia, niombe Manispaa hiki ni chanzo kipya cha mapato, hakikisheni
fedha za wananchi ziingizwe moja kwa moja kwenye akaunti yake wakati wa mauzo
ambayo ataiwasilisha Manispaa wakati wa uundaji mkataba” Amesema RC Mwassa.
Kwa upande
wa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Albert Masando,amesema kwa sasa Mji
unahitaji kupangwa hivyo wananchi lazima wasikilize maelekezo na maagizo ya
Viongozi badala ya kukiuka maagizo hayo.
Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Ally Machela,amesema katika mchanganuo wa matumizi ya viwanja , eneo la makazi Viwanja 2,740, Makazi na Biashara 915, Huduma (Shule, Zahanati, Vituo vya afya n.k) 147, Biashara 36, Viwanda Vidogo 68 na Maeneo ya wazi (POS) na Viwanja vya Michezo 59.
Zoezi la
Ugawaji wa Fomu za mauzo ya Viwanja litaanza kufanyika Tarehe 5/12/2022 katika
Ofisi za Ardhi zilizopo Stendi Mpya ya Daladala Mafiga ambapo kwa malipo ya
ununuzi ya Viwanja yatafanyika kwa awamu moja ndani ya miezi 3 na bei ya fomu
ni shilingi elfu 20.
Post a Comment