Header Ads

DKT. MPANGO AAGIZA WAKUU WA MIKOA KUDHIBITI UHARIBIFU WA MAZINGIRA.




MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amewataka wakuu wa mikoa, viongozi wa Wilaya na Bodi za Mabonde ya Maji nchini kuhakikisha wanadhibiti uharibifu wa mazingira unaosababishwa na shughuli za kibinaadamu jambo ambalo linachangia upungufu wa kina cha maji katika mito hapa Nchini.

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango ametoa maagizo hayo Novemba 9, 2022 alipotembelea mitambo ya uzalishaji wa Maji Ruvu chini iliyopo mkoa wa Pwani na kisha kupokea taarifa ya hali ya uzalishaji na upatikanaji wa maji katika mikoa ya Dar es na Pwani.

Aidha, Makamu wa Rais ameitaka Wizara ya Maji kushirikiana na Tamisemi kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya uchimbaji wa visima vya maji na mabwawa ili kupunguza changamoto ya upatikanaji wa maji hapa nchini.

Sambamba na hayo Makamu wa Rais amekemea vitendo vinavyofanywa na baadhi ya wananchi wasiokuwa waadilifu wanaochoma misitu kwa ajili ya kuandaa mashamba huku akitoa wito kwa wananchi wote kuachana na tabia hizo za uchafuzi wa mazingira kando kando ya vyanzo vya Maji.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.